Na Khadija Kalili
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani kupitia Kamanda wa Mkoa RPC Wankyo Nyigesa ameanzisha michuano ya Kombe la Uhalifu Haulipi 2021 kwa lengo la kupunguza vitendo vya Uhalifu ndani ya Mkoa wa Pwani.
RPC Wankyo alisema hayo leo katika uzinduzi wa michuano hiyo uliofanyika leo jioni katika viwanja vya Bwawani Kibaha Mkoani Pwani ambapo michuano hiyo itazishirikisha timu za watu kutoka katika kada mbalimbali pamoja na timu 16.
Michuano imeandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa ushirikiano na Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kibaha (KIBAFA).
Alizitaja timu hizo ambazo zitashiriki katika michuano hiyo ni Bodaboda FC, Bwawani FC, Gereji, Hisia Kali FC, Juhudi FC, Kiswamba Electronicnics FC, Matunda FC, Mali Asili FC, Mlandizi Combine FC, Mailimoja FC, Wagosi FC, Wajeda FC, Wakulungwa FC, Tangini FC na Visiga FC.
Aidha RPC Wankyo alisema kuwa michuano hiyo itafanyika ndani ya wiki mbili huku timu hizo zikichuana katika mzunguko wa mtoano ambapo fainali itarindima Oktoba 16 mwaka huu katika Uwanja wa Bwawani Kibaha.
Alizitaja zawadi zitakazotolewa ni ng'ombe na kiasi cha Sh. 100,0000kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata Mbuzi na kiasi Cha Sh. 100,000 watakaobaki watashikwa mkono.
Aidha aliyekuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano hiyo amewaagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Kibiti waanzishe mashindano kama haya Ili waweze kuunda timu moja itakayo uwakilisha Mkoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...