Na Damian Kunambi, Njombe

Wananchi wa kata ya Ibumi iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe wamemshukuru rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza fedha za ununuzi wa mahindi sambamba na kuwasilisha ombi la kuongezewa tani nyingine zaidi.

 Wakiwasilisha ombi hilo mbele ya mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga wananchi hao wamedai kuwa awali chama chao cha ushirika kilipewa nafasi ya kuuza tani 50 na awamu hii wamepatiwa tani 100 kitu ambacho bado hakikidhi haja ya wakulima.

Lamon Komba ni katibu wa chama cha ushirika kijiji cha Ibumi amesema chama hicho kina wanachama 134 ambapo kwa mgawanyo wa tani hizo zilizotolewa ni sawa na gunia 10 kwa kila mwanachama kitu ambacho bado hakijakidhi haja ya wakulima.

"Tunaomba serikali itusaidie kwani bei ya mtaani si nzuri tunauza debe moja kwa elfu tatu kiasi ambacho hakirudishi gharama za kilimo tulizotumia hivyo tunaiomba serikali itusaidie tena kuongeza fedha za ununuzi kwakuwa maisha yetu tunayaendesha kwa kutegemea kilimo hiki ". Amesema Komba.

 Edward Haule ni diwani wa kata hiyo amesema bado wananchi wana mahindi mengi majumbani mwao na wengine yapo mashambani bado hawajavuna hivyo mahindi hayo yote yamekosa soko.

"Ukipita kwenye nyumba za watu unakutana na marundo ya mahindi tu! hapo bado mengine hayajavunwa mashambani hivyo yatakapovunwa nayo yatazidi kujazana pasipo kuwa na soko la uhakika",

Aidha kwa upande wa mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga amesema tatizo hilo lipo katika kata nyingi za wilaya hiyo na anafahamu kwa jinsi gani wakulima hao wanaumia kwa kukosa soko hivyo ataendelea kupambana kutafuta soko la mahindi hayo.

Ameongeza kuwa wananchi wa jimbo lake shughuli zao kubwa ni kilimo cha mahindi na wananchi hutegemea fedha za mahindi kwa kusomesha watoto wao na kufanya maendeleo mengine.

"Ninaposikia wakulima wamekosa soko la mahindi huwa naumia sana kwakua najua athari wanazozipata, mimi nimesomeshwa kwa fedha za mahindi na nilikuwa namuona mama yangu anavyohangaika kutafuta soko ili niweze kupata ada ya shule na ndiomaana nahangaika sana juu ya wakulima". Amesema Kamonga.

 

Mbunge wa jimbo wa Ludewa Joseph Kamonga akipokea zawadi ya mkungu wa ndizi kutoka kwa wananchi wa kata ya Ibumi
Diwani wa kata ya Ibumi Edward Haule akiongea na wananchi mara baada ya kufanya ziara katani hapo
Wananchi wa kata ya Ibumi wakifuatilia mkutano wa mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga baada ya kufanya ziara katika kata hiyo
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akisoma changamoto mbalimbali za wananchi wa Ibumi alizoziandika katika kitabu chake na kuzijibu
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kulia) akipokea zawadi ya Tangawizi kutoka kwa wakulima wa kijiji cha Ibumi.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...