WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imesema bado ulaji wa nyama nchini Tanzania ni mdogo ambapo kwa sasa ulaji ni kilo 15 kwa mtu tofauti na tafiti za shirika la chakula Duniani linaloelekeza kila mtu atumie kilo 50 kwa mwaka.
Akizungumza, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Amosy Zephania katika ziara yake ya kikazi katika shamba la kuku la Irvine wilayani siha Mkoani Kilimanjaro Septemba 21,2021 ambapo alisema kuwa kutokana na hali hiyo serikali inatarajia kuendelea kutoa elimu kwa watanzania kuona umuhimu wa ulaji wa nyama .
“Sensa ya mifugo ya mwaka 2019/2020 inanyesha katika kaya zinazijishughulisha na kilimo na ufugaji Tanzania ni zaidi ya milioni saba, kaya zaidi ya milioni nne sawa na asilimia 55. 3 wanafuga kuku kuanzia 10 na kuendelea, hii inaonyesha jinsi tunavyozungumza kuku tu, nazungumzia maisha ya watanzania kwanzia ngazi ya chini hadi juu, "amesema
Amesema ni wajibu wa Kampuni hiyo kuhamasisha wananchi kujikita katika ufugaji wa kuku hali itakayo peleka ongezeko la ulaji wa nyama kwa watanzania.
" Toeni elimu kwa jamii, jitanganezi, zipo pesa katika kila halmashauri nchi nzima fikeni huko, zungumzeni na wakurugenzi wakopesheni kuku vijana, kinamama, watu wenye ulemavu, uwezo wa kulipa upo, kwa kufanya hivyo tutawafikia watanzania wengi zaidi na ulaji wa nyama utaongezeka, "amesema
Kwa upande wake meneja masoko na uendelezaji wa biashara wa Kampuni hiyo nchini, Jeremia Kilato amesema wanazalisha vifaranga zaidi laki 220 kwa wiki, ingawa wanatarajia kuongeza uzalishaji hadi kufikia zaidi ya laki 290 kwa wiki.
" Tunajivunia uzalishaji wa kisasa na wenye ubora wa kimataifa, lakini kwa sasa tunakabiliwa na changamoto, ni ongezeko kubwa la uhitaji wa vifaranga hasa katika kipindi hichi cha Uviko 19, Kampuni imeweka mikakati ya kuweza kununua mashine mpya itakayoongeza uzalishaji kutoka 220 hadi 290,"amesema.
Amesema, wanatarajia kuendelea kusambaza vifaranga katika Wilaya zote na Mikoa yote ambapo hadi sasa tayari wamesambaza katika mikoa 13.
Kwa upande wake meneja wa kituo cha
uwekezaji Kanda ya Kaskazini, Bw. Daudi Riganda amesema mwekezaji huyo yupo kihalali na yupo kwenye hatua za mwisho.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Amosy Zephania akiongea na watendaji wa shamba la irvine's (hawapo pichani) lililopo Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani huko September 21,2021 lengo ni kuona namna wanaendesha shughuli zao na kisikiliza changamoto zinazowakabili na kuzifanyia kazi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Amosy Zephania (waliokaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa shamba la irvine's wa pili kutoka kushoto ni Darryl Combe na wa pili kutoka kulia ni Fabio Stella pamoja na watumishi wa shamba hilo na watumishi kutoka Wizara ya Mifugo na uvuvi , mara baada ya kutembelea shamba hilo lililopo Siha Mkoani Kilimanjaro. Septemba 21,2021
Meneja wa nchi wa shamba ufugaji wa kuku Irvine's, Darryl Combe akieleza namna shamba lao lilivyoanza hadi kufikia sasa na malengo yao katika kuendelea kukuza shamba ilo wakati wa ziara ya Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Amosy Zephania (hayupo pichani) kwenye shamba hilo Mkoani Kilimanjaro Septemba 21,2021
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...