Waziri wa Kilimo, Prof Adolf
Mkenda akisisitiza jambo wakati wa kikao cha wadau wa ubanguaji wa korosho
kilichofanyika mkoani Mtwara, jana, kikiwa na lengo la kutatua changamoto
zinazowakabili wadau hao, Tarehe 20 Septemba 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo, Prof Adolf
Mkenda akisisitiza jambo wakati wa kikao cha wadau wa ubanguaji wa korosho
kilichofanyika mkoani Mtwara, jana, kikiwa na lengo la kutatua changamoto
zinazowakabili wadau hao,
Sehemu ya wadau wa ubanguaji
wa korosho wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao chao na
Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda kilichofanyika mkoani Mtwara, jana, kikiwa
na lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wadau hao,
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akisisitiza juu ya umuhimu wa ushirikiano baina ya wadau wa ubanguaji wa korosho wakati wa kikao cha wadau hao kilichofanyika mkoani Mtwara, jana, kikiwa na lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wadau hao, Tarehe 20 Septemba 2021.
Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, Francis Alfred akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa ubanguaji wa korosho kilichofanyika mkoani Mtwara, jana, kikiwa na lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wadau hao, Tarehe 20 Septemba 2021.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
WAZIRI wa Kilimo, Prof Adolf
Mkenda amewataka wabanguaji zao la korosho kuja na mikakati itakayowezesha zoezi hilo kufikia asilimia 60
au 100 ifikapo mwaka 2025.
Waziri Mkenda ameyasema hayo
mjini Mtwara wakati akizungumza na wadau wa ubanguaji Korosho kwenye mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapo.
Amesema kuwa madhumuni ya
kikao hicho ni kushauriana kujenga mwelekeo wa kuhakikisha kwamba adhma inafikiwa
ya walau kwa kima cha chini kabisa asilimia 60 ya korosho ibanguliwe hapa
nchini.
“Na hicho ni kima cha chini
kabisa ikifika mwaka 2025 maana kima cha chini kabisa ni kwamba tukifika
asilimia 100 tena ndio tutafurahi zaidi sasa kwa kasi ambayo tunakwenda nayo ni
vizuri tukawa tunashauriana kwa maana 2025 ni kesho tuu,”.
Amesema kuwa kwa sasa ni
asilimia 10 tu ya korosho inabanguliwa hapa nchini na ubora umeongezeka na
ladha imekuwa nzuri zaidi Lakini linahitajika soko kubwa la nje kwa kuwa fedha
nyingi zipo huko.
“Tukiweza kuwauzia wale
sababu kipato na fedha zipo huko nyingi, wakulima watakuwa na fedha nyingi
zaidi na kutakuwa na ajira za kutosha nchini hasa maeneo ya Mtwara na Lindi na
Serikali itapata fedha,”.
Alibainisha ni changamoto
inayotakuwa kufanyiwa kazi kwa
kushirikiana na wadau wote kwakuwa Serikali haiwezi kutekeleza yenyewe kwa
kukaa ofisini.
Naibu Waziri wa kilimo, Mhe
Hussein Bashe amesema kuongeza thamani kwenye zao hilo ni jambo la msingi
husuani kwenye ubanguaji.
Amesema zipo changamoto za
riba kwenye zao hilo ambapo Rais ametoa Trilioni moja kwa ajili ya kwenda
kwenye shughuli za kiuchumi zitakazokopeshwa chini ya asilimia 10 na taasisi za
fedha.
Amesema changamoto
wanayokabiliana nayo wabanguaji ni mitaji kwamba kiwanda kina uwezo wa
kuchakata tani 10 kwa siku maana yake kwa mwezi ni tani 300 hivyo ili kufanye
kazi mwaka mzima kinahitaji zaidi ya tani 3,600.
Amebainisha kuwa zipo
changamoto za kisera ambazo zimeshaanza kufanyiwa kazi kwa kushirikiana na
taasisi mbalimbali za fedha ili wabangue korosho kwa kiasi kikubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...