Na Mwandishi wetu Mihambwe
Wakazi
Tarafa ya Mihambwe wamehasika vilivyo kwa hiyari yao kupata chanjo ya
Uviko 19 (Corona) mara baada ya kuelimishwa na huduma kusogezwa jirani
na Wananchi.
"Nashukuru
sana kupata chanjo ya Corona, niwaombe Watanzania wenzangu tuendane na
Dunia ilivyo, na sidhani kuna Mtanzania ama kiongozi yeyote yule anataka
kuwatesa Wananchi. Tuchanje ili kupunguza madhara ya ugonjwa huu."
amesema Ndaile Abdallah Ulaya mkazi Kijiji cha Dinyeke
Muuguzi
Asha Kasembe amewahimiza akina Mama na Wananchi wote wapate chanjo
kwani ni salama na inaimalisha kinga za mwili na kupunguza vifo na
inapunguza makali.
Pia
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ameungana na Rais Samia kupambana
na ugonjwa huu kwa kuwapa elimu Wananchi, kuwahamasisha na wanaoridhia
wanapata chanjo bure.
"Dunia
ipo kwenye mapambano ya Uviko 19 nasi Tarafa ya Mihambwe tunaungana na
Rais Samia kupambana na ugonjwa huu kwenye vijiji na vitongoji
kuwaelimisha, kuwahamasisha na tumeona Watu wengi wamejitokeza kwa
hiyari yao kupata kinga kutokana na huduma ya chanjo kuwafikia jirani
nao. Nazidi kusisitiza Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe tuendelea kuchukua
tahadhari ya ugonjwa huu wa Corona kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa
vitakasa mikono, kuepuka mikusanyiko na kupata chanjo ya sindano ya
Corona" alisisitiza Gavana Shilatu.
Katika
zoezi hilo Mamia ya Wananchi wamejitokeza kupata chanjo ya Corona na
zoezi hilo litakuwa endelevu ndani ya Tarafa ya Mihambwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...