Na Mwandishi Wetu, Ufaransa
UBALOZI wa Tanzania nchini Ufaransa umefanya mkutano wa wadau wa utalii Ubalozini kwa madhumuni ya kuwahakikishia wadau hao utayari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kupokea Watalii hususan kwa wakati huu baada ya dunia kukumbwa na janga la ugonjwa wa Corona ambao umeathiri sana sekta ya utalii duniani kote.
Aidha,katika mkutano huo, uliofanyika Septemba 9,2021 Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Samwel Shelukindo alifahamisha wadau hao kuhusu juhudi zinazofanywa naSamia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ameamua kufanya ziara iitwayo "Royal Tour"katika maeneo makubwa yenye vivutio nchini Tanzania.
Balozi Shelukindo aliwaeleza wadau kwamba jitihada hizo zinalenga kuitangaza Tanzania upya (Rebranding) na vivutio vyake vya utalii. Takriban wadau 60 walishiriki mkutano huo ambapo miongoni mwao ni makampuni makubwa yanayojihusisha na utalii (Tour Operators), Waandishi wa habari wanaotangaza utalii, Wafanyabiashara.
Wakati huo huo, Ubalozi unaratibu ziara ya kundi la Watalii 77 wanaotegemea kwenda Tanzania kuanzia tarehe 7 mpaka 12 Oktoba 2021 kutembelea maeneo mbalimbali.
Home
UTALII WETU
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA WAHAKIKISHIA WADAU UTAYARI SERIKALI AWAMU YA SITA KUPOKEA WATALII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...