Na Sixmund J. Begashe.

 

Ujerumani kuendelea kushirikiana na Mkumbusho ya Taifa katika nyanja ya Utafiti, maonesho, kubadilishana uzoefu na program mbalimbali ili kuendeleza uhifadhi wa urithi wa kihistoria, Mambokale na utamaduni kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho

 

Kikao hicho maalum Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika kutoka nchini Ujerumani Bw Robert Doelger aliye ambatana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Mhe Regina Hess kililenga katika kuyatazama mashirikiano ya sasa na kuona fursa zaidi za mashirikiano mengine.

 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makumbuaho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema kuwa wana matarajio makubwa kutokana na ujuio wa Mhe Doelger kwani katika mazungumzo yao wamegundua kuwa ipo mikusanyo mingi ya kihistoria iliyotoka Afrika hususani Tanzania ambayo imehifadhiwa nchini Ujerumani ambayo haikujulikana huko nyuma, hivyo itapanua wigo wa mashirikiano na taasisi zenye mikusanyo hiyo.

 

Naye Balozi wa Ujerumani Nchini Mhe Regina Hess ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa jitihada mbalimbali inazozichukuwa katika kuhifadhi urithi wa kistoria, wa Mambokale na wakiutamaduni ambao ni muhimu zaidi kwa kuelimisha jamii juu ya mahusiano kati ya Tanzania na Ujerumani.

 

Tumepata nafasi nzuri ya kuzungumza na uongozi wa Makumbusho ya Taifa juu ya Mambo muhimu yanayohusu mashirikiano katika uhifadhi wa urithi wa Historia, pia mgeni wetu Mhe Doelger amefurahi sana kuona maonesho mbalimbali ya chimbuko la Mwanadamu, Historia, Sanaa nk, tuliona tumlete hapa ili ajionee mwenyewe maana sisi tumesha fika hapa mara kadhaa” Alisema Balozi Hess.

 

Mkuu wa Idara ya Program Bwana Chance Ezekiel, amesema ujio wa wageni hao umezidi kufungua milango ya mashirikiano hasa katika mausala ya program mbalimbali hususani za Sanaa kwani hadi sasa yapo mahusiano mazuri kati ya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na kituo cha Utamaduni cha Ujerumani hapa nchini.

Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika kutoka nchini Ujerumani  Bw Robert Doelger alifafanua jambo kwenye mazungumzo yake na uongozi wa Makumbusho ya Taifa (haupo pichani).
Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika kutoka nchini Ujerumani Bw Robert Doelger, ujumbe alioambatana nao na viongozi wa Makumbusho ya Taifa wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mkumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga
Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika kutoka nchini Ujerumani  Bw Robert Doelger akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga, alipo itembelea Taasisi hiyo
Kushoton ni Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika kutoka nchini Ujerumani  Bw Robert Doelger, Mkurugenzi Mkuu wa Mkumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga, Balozi wa Ujerumani hapa nchini  mhe Regine Hess (kushoto), baada ya ugeni huo kuwasili Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika kutoka nchini Ujerumani  Bw Robert Doelger na Balozi wa Ujerumani hapa nchini  mhe Regine Hess ( kushoto) wakilitazama fuvu la binadamu wa kale  Zinjanthropus anaesadikiwa kuishi Miaka milioni 1 lakini saba iliyo pita 

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...