Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo imetakiwa kuboresha tamasha la Tanzanite ili kuwa kivutio kwa sekta ya utalii na masuala ya kidiplomasia.
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Jenista Mhagama amesema amesema michezo ni sekta kubwa na inakuwa kwa kasi kubwa na kutoa ajira kwa vijana.
Jenista amesema, serikali kupitia wizara imejipanga kutanua wigo wa utalii wa utamaduni na michezo Ili kuvutia na kuiboresha zaidi sekta hiyo.
“ serikali kupitia wizara imejizatiti katika kutanua wigo wa utalii kwa kuboresha zaidi ambapo kila mwaka timu au wawakilishi wakiwa wanafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa watakuwa wanasaidia kutangaza vivutio vyetu,” amesema Jenista.
“Wizara iongeze ufanisi ili kuikuza sekta ya michezo na utalii kwa pamoja, kwa sababu michezo ni sekta kubwa inayotoa ajira kwa vijana,” amesema
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amesema
alisema anaishukuru wizara kufanya tamasha hilo ndani ya wilaya hiyo.
Amesema mtoto wa kike anatakiwa kuwa na imani na fusra ambazo anapata kwa kuwa mwanamke ni tumaini la kila mmoja.
"Mtoto wa kike anathaminiwa kila mmoja, naomba kila mmoja ajithamini kwa kuwa ana nafasi ya kufanya lolote, popote cha msingi ni ajithamini tu," amesema.
Tamasha hilo limehitimishwa leo ambapo michezo mbalimbali iliweza kuchezwa ikiwemo kukuna nazi, rede, mpira wa miguu, mpira wa pete, kikapu, kuvuta kamba na michezo ya jadi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...