Na Daudi Manongi
Wachimbaji wa madini nchini wameaswa kufanya
shughuli zao za uchimbaji kwa upendo ili kuepuka migogoro ya mara kwa
mara na kesi zisizoisha katika maeneo ya uchimbaji.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Madini Mhe.Prof.Shukrani Manya wakati
akitatua mgogoro wa wa umiliki wa mgodi wa uchimbaji dhahabu katika
machimbo ya matongo Wilayani Ikungi.
“Maelekezo ya Serikali ni
kwamba mnapaswa kuchimba kwa usalama lakini pia kwa kupendana,Wizara
yetu sio ya migogoro bali tupo hapa kwa ajili ya kutoa huduma kwa
wachimbaji ili kuleta tija katika masilahi yenu binafsi na maendeleo ya
uchumi wa taifa hili”,amesema.
Akitoa elimu kwa wachimbaji hao
kuhusu umuhimu wa leseni Prof Manya alisisitiza wachimbaji hao kufika
kwa afisa madini mkazi ili waombe leseni za uchimbaji wa madini.
“Kabla
ya kuanza kuchimba madini unaitaji kukatia leseni eneo hilo hili
ujulikane unamiliki ardhi juu na madini yaliyoko chini ili yaweza kuwa
ni halali yako”amesisistiza
Aidha Naibu Waziri Prof.Manya
aliwaasa wachimbaji na wamiliki wa leseni kumshirikisha Afisa madini
mkazi katika kila jambo wanaloona hawalielewi na lina utata ili
kupunguza migogoro.
Katika hatua nyingine amewata wachimbaji hao kushiriki katika masuala ya kijamii ili kijiji icho kinufaike na uwekezaji wao.
“Nawaasa
changieni madawati katika elimu,tumekuja kutafuta riziki katika kijiji
hiki mkiondoka hapa Mashimo yatabaki hapa kwa iyo wenye Mwalo,mwenye
karai na mwenye leseni ikitokea hoja ya kijiji iwe hoja yenu
wote”ameeleza.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Bw.Jerry
Muro altoa wito kwa wachimbaji hao kudumisha Amani na kujikinga na
uviko-19 na pia kuwaamasisha kujitokea kupata chanjo kwani wamesogeza
vituo katika eneo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...