Wizara ya Madini
imeipongeza kampuni ya kitanzania ya Javan Investiment and Co Ltd kwa
kutumia utaalamu waliosomea nchini kuwekeza katika utafutaji wa madini
ya Almasi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Madini
Mhe.Prof.Shukrani Manya wakati alipotembelea kampuni iyo kukagua
maendeleo ya mradi huo katika eneo la mberekese,Iramba.
“Siku
zote tumekuwa tukiamini kwamba uwekezaji mkubwa wa utafutaji madini
nchini lazima uhusishe kampuni za kigeni,lakini hawa wanatoa mfano hai
wa namna ambavyo mtanzania anaweza akasoma na kuweka uzoefu wake wa
kufanya kazi katika kampuni tofauti na akaanzisha kampuni yake ya
uwekezaji katika shughuli za madini na matokeo yake ndo tunayaona hapa”,
amesema.
Ameongeza kuwa kuanzishwa kwa mgodi huo nchini utakuwa ni mgodi mwingine mkubwa wa kitanzania ambao utazalisha almasi kwa wingi.
Ametoa rai kwa watanzania kuthubutu kufanya shughuli ambazo zinausisha uwekezaji mkubwa kwani uwezo wanao
Aidha
amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Iramba kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini
mkazi ili kushughulikia migogoro ya uchimbaji wa madini kwani
litasaidia kutatua migogoro iyo kwa haraka ili kazi za uchimbani wa
madini ziendele na mapato yapatikane.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Iramba,Suleiman Mwenda amesema wamefarijika na ugeni huo na
lengo lao kubwa kwa sasa kama wilaya ni kuongeza uzalishaji wa madini
ambapo kwa msimu uliopita walizalisha gramu 317000 na kuingiza bilioni
36 kutoka katika madini ya dhahabu kwa ujumla.
“Kwa sasa tuko
katika kuongeza wigo wa wawekezaji zaidi wa madini kwani tuna maeneo
mengi yenye dhahabu katika Wilaya yetu ili tuongeze uzalishaji na tuna
watu zaidi ya elfu kumi ambao wamejiajiri kwenye uchimbaji na pia kwa
sasa tunakusanya mapato yetu katika eneo hilo maana utachangia katika
ucumi wetu kwa ujumla”,ameongeza.
Naye mwekezaji wa Mgodi huo
Bw.Javan Bidogo amesema wameshukuru kwa ujio wa Naibu Waziri uyo kwani
umewatia nguvu kuona Serikali iko karibu nao na inawapa ushirikiano wa
kutosha,amesema mgodi huo mpaka sasa umeajiri wafanyakazi 50 katika
kipindi hiki cha utafiti lakini wakifikia kipindi cha uzalishaji
wataajiri wafanyakazi 1000 patika kila mgodi watakaokuwaa wameanzisha.
kwa sasa nchini migodi mikubwa ya Almasi inahusisha mgodi wa mwadui ambao upo tangu miaka 1940 na mingine ni midogo sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...