Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limesema kupitia kwenye kituo chake cha Mfano cha wachimbaji wadogo kilichopo eneo la Lwamgasa Mkoani Geita wameweza kuwafikia wachimbaji wadogo zaidi ya 200 kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwahudumia katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya uchenjuaji.
Hayo yamesemwa na Meneja Mwendeshaji wa kituo hicho Victor Augustine kwenye ziara ya wadau wa sekta ya madini walipotembelea kituo hicho kwaaajili ya kujifunza na kufahamu namna ambavyo kituo hicho kinavyofanya shughuli zake.
Amesema Kituo hicho mpaka sasa kimeweza kuwasaidia wachimbaji zaidi ya 200 ambao wamefika kwaajili ya kupata elimu ya kitaalamu kuhusu mambo mbalimbali ya uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu pamoja na kuwahudumia kwa kuchenjua dhahabu yao kwa gharama nafuu.
“Pamoja na kutoa elimu pia tunachenjua dhahabu zao na kusimamia zoezi zima mpaka hatua ya mwisho ya kukabidhiwa dhahabu yake pamoja na kuwapa ushauri wa kitaalamu kwenye sekta hii ambayo imewasaidia sana na kuendelea kukiamini Kituo chetu," amesema Victor.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya HEXAD, Fortunatus Luemeja akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo mkoani humo ameishukuru STAMICO kuwajengea Kituo hicho ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwao wa kufanya shughuli zao wakiwa na uhakika wa kupata dhahabu yenye viwango vya juu na kuweza kuipeleka kwenye soko la dhahabu kulingana na bei elekezi ya soko hilo.
“Kituo hiki ni muhimu sana kwetu sisi wachimbaji wadogo kinatusaidia sana kutokakana na ufanisi wake wa kazi na uwazi kwenye zoezi zima la kuchenjua lakini ipo changamoto ya udogo wa kituo hii inasabibisha kuchukua muda mrefu hadi mwezi mmoja pale unapokuwa na mzigo mkubwa,” amesema Luemeja.
STAMICO ni Shirika la Madini la Taifa lenye majukumu ya kusimamia shughuli za uchimbaji wadogo katika migodi ya Serikali, kuwalea na kuwaendeleza wachimbaji wachimbaji wadogo pamoja na kufanya utafiti na shughuli za uchorongaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...