Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI
la Polisi mkoa wa Kipolisi Rufiji ,linawashikilia watuhumiwa wawili kwa
kukutwa na nyara za serikali, zinazodaiwa ni meno ya tembo , uzito wa
kilo 25.
Kaimu kamanda wa
polisi mkoa wa kipolisi Rufiji ACP Protas Mutayoba alisema ,tukio hilo
limetokea usiku wa kuamkia Jana huko maeneo ya Utunge-Kisemvule
wilayani Mkuranga.
Mutayoba
alieleza kuwa, waliwakamata watuhumiwa hao wawili mmoja ni mwanaume
mwenye umri wa miaka 40 na mwengine ni mwanamke mwenye umri wa miaka 21
,wakiwa na nyara za serikali zidhaniwazo kuwa ni meno ya tembo vipande
16 vyenye uzito wa kilo 25 ambapo thamani yake haijajulikana.
Aidha
Kamanda Mutayoba alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi la
polisi kwa uchunguzi zaidi na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Katika
hatua nyingine ,Kamanda Mutayoba alieleza, huko kitongoji cha
Matope-Kimanzichana wilayani Mkuranga jeshi la polisi limemkamata
mtuhumiwa mmoja mwanaume,akiwa na kilogram 150 za bangi ambapo mtuhumiwa
huyo ameshafikishwa mahakamani kwa kosa la kupatikana na bangi.
Aidha
jeshi la polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi wote kutoa
ushirikiano kwa jeshi la polisi na kuwaasa wananchi kuacha tabia ya
kufanya biashara haramu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...