Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Mwenyekiti
wa kamati ya Usalama mkoa wa Pwani,Abubakari Kunenge ameeleza watu 16
waliohujumu miundombinu ya mradi wa reli ya kisasa (SGR) pamoja na
wengine kuiba saruji katika mradi mkubwa wa umeme Stigo Rufiji
wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Aidha ameagiza watendaji waliopo katika maeneo ya mradi wa SGR kutoa taarifa haraka pale watakapobaini wabadhilifu.
Aliweka
bayana hayo wakati alipoambatana na kamati ya Usalama mkoa,wakuu wa
wilaya ,maDAS kutembelea daraja la kisasa (WAMI ) na karakana na
stesheni ya kupokea mizigo kituo Cha Pugu(SGR) ambapo Kunenge ,alitaka
ulinzi uimarishwe kwenye maeneo yote ya miradi ya kitaifa iiliyopo
Pwani.
Alitaja waliohujumu kanda ya kipolisi Rufiji wapo 11 na Pwani wapo watano.
Kunenge
aliwaelekeza wakuu wa Wilaya mradi wa SGR unapopita kuitengeneza kuwa
miji na mazingira bora iweze kuendana na mradi huo.
"SGR
mradi mkubwa na muhimu yapaswa kulindwa na kuongeza mradi huu unakwenda
kuondoa msongamano wa magari na kupunguza ajali barabara kuu ya
Morogoro-Pwani-Dar es salaam".
"Matarajio
yetu treni hii ya umeme kuanza kazi mwezi wa kumi na moja ili
kunufaisha wananchi kwa kurahisisha usafiri na kufika kwa muda mfupi "Na
kuomba jamii isaidie kulinda miundombinu ya Mradi.
Nae mhandisi Tadei Kamu alifafanua,mradi huo umefikia asilimia 93 ,kipande cha DaresSalaam-Morogoro Trilioni 2.7.
Wakati huo huo,akiwa mradi wa Daraja WAMI Kunenge alimuelekeza mkandarasi kukamilisha wakati alioomba kuongezwa Tena kwa wakati.
Alisema
,daraja la WAMI la zamani lilijengwa 1959 na ni kiungo kutoka Chalinze
kwenda mikoa ya Kaskazini mwa nchi yetu na nchi jirani .
"Daraja
hilo halikidhi mahitaji ya magari yanayopita kwa kuwa lilijengwa miaka
mingi iliyopita na ni jembamba lenye njia moja, barabara zinazounganisha
daraja hili ziko kwenye miinuko mikali na kona mbaya ambapo ajali mbaya
na vifo vimekuwa vikitokea mara kwa mara ,"
"Nimekuja
na nyie wote kwakuwa ni timu moja ya mkoa ninayofanya nanyi kazi muone
yanayofanyika chini ya serikali yetu ya Rais Samia,na kauli mbiu yetu ni
PWANI YA SAMIA TIMU MOJA KAZI IENDELEE"
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete alisema mradi huo umetengeneza
ajira 500 ,za vijana aliishukuru serikali na Rais Samia Suluhu kwa
juhudi zake.
Alisema,
Daraja jipya likikamilika litakuwa kubwa urefu wa mita 510 na upana wa
mita 11.85 linajengwa umbali wa mita 670 pembeni mwa daraja la zamani .
Ridhiwani
alieleza ,daraja hili litakuwa na uwezo mkubwa katika usafirishaji na
kufungua milango ya kimaendeleo na kukuza uchumi Chalinze na nchi yetu
kijumla.
Awali akitoa taarifa ya mradi ,meneja wa TANROADS Pwani ,Andrea Kasamwa ,alisema mradi umefikia asilimia 64 .
Alieleza
, Mkandarasi alianza kazi ya Ujenzi 22,octoba 2018 na kutakiwa
kukamilisha mradi September 2021 miezi 35 lakini Mkandarasi amewasilisha
sababu za kimkataba nyongeza ya muda wa ujenzi kufika 2022.
Kasamwa
alieleza, hivi karibuni Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi ,Pro.Makame
Mbarawa alimuagiza Mkandarasi Power Construction Corporation Ltd kutoka
China.
Alisema ,tayari
mkandarasi huyo ameongeza kasi ya kufanya kazi ikiwa ni agizo la waziri
huyo kwa kuongeza raslimali watu watumishi kutoka 230 hadi 520 na kasi
ya mtambo mara mbili na mafundi wa zamu mchana na usiku .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...