Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money leo imetangaza HABARI NJEMA kwa wateja pamoja na Mawakala kwa kutoa faida ya TZS2.1bn kuanzaia leo. Faida hiyo ni kwa kipindi cha robo mwaka ya April hadi June 2021 na mteja anaweza kutumia gawio la faida analopata kulipia huduma au bili mbali mbali atakavyo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati kutangaza HABARI NJEMA na Airtel Money, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema, ‘Tunayo furaha siku ya leo tena kwa kutoa faida kwa wateja pamoja na Mawakala wetu huku tukishuhudia huduma yetu ya Airtel Money ikikua siku hadi siku. Leo Airtel Money inatangaza kutoa faida ya TZS2.1bn kwa wateja pamoja na Mawakala wa Airtel Money na kila mteja na Wakala atapata faida kulingana na matuzi yake ya huduma ya Airtel Money kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia Aprili hadi juni 2021”. Nchunda alisema.
‘Nia yetu sisi kama watoa huduma ni kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwenye suluhisho la kifedha hapa nchini. Faida wanayopokea wateja wetu leo pamoja na Mawakala ni kutokana na matumizi yao ya huduma yetu ya Airtel Money. Nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania waendelee kutumia huduma ya kampuni yao ya Airtel Money kwani inapatikana kwa urahisi, nafuu na salama’, alisema Nchunda.
‘Tunayo furaha kwani licha ya kutoa faida kwa wateja wetu, pia zaidi ya Mawakala 100,000 nao watapa faida yao moja kwa moja kupitia akaunti zao za Airtel Money. Nawaomba Mawakala wetu popote walipo waendelee kuwahudumia wateja wetu kwa kuwapa huduma iliyo bora kabisa kwani wana uhakika wa kupata faida kwa robo ya kila mwaka’, Nchunda aliongeza.
Kwa upande wake, Meneja uhusianao wa Airtel Jackson Mmbando alisema, ‘Airtel imedhamiria kuendelea kutoa huduma zilizo bora kabisa za Airtel Money pamoja na kusogeza huduma hizi karibu na wateja watu na hivyo kuwafikia wengi ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki. Kwenye suala la kuwa suluhisho la kifedha hapa nchini, Airtel hivi karibuni ilizindua huduma ya TUMA PESA BURE, huduma ambayo inawapa fursa wateja wa Airtel Money kutuma pesa bure Airtel kwenda Airtel.
Airtel money ni huduma kabambe kwenye kufanya malipo kidigitali, imekuwa ikija na huduma za kibunifu mara kwa mara kwa lengo la kutoa huduma bora na nafuu kwa watanzania wote. Airtel Money tayari imeunganishwa na huduma za malipo zaidi ya 1000 zikiwemo malipo ya bili pamoja na huduma za malipo ya serikali huku pia ikiwa imeunganisha na zaidi ya benki 40 nchini ili kuwezesha malipo na uhamishaji wa miamala kuwa rahisi wakati wowote .
Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda akitangaza kutoa faida ya TZS2.1bn kwa wateja pamoja na Mawakala wa Airtel Money kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia Aprili hadi juni 2021, kila mteja na Wakala atapata faida kulingana na matuzi yake ya huduma ya Airtel Money,pichani kushoto ni Meneja uhusianao wa Airtel Jackson Mmbando
Meneja uhusianao wa Airtel Jackson Mmbando akifafanua jambo mara baada ya kutangaza kutoa faida ya TZS2.1bn kwa wateja pamoja na Mawakala wa Airtel Money kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia Aprili hadi juni 2021, kila mteja na Wakala atapata faida kulingana na matuzi yake ya huduma ya Airtel Money,pichani kulia ni Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...