Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

WABUNIFU wa Mavazi hapa nchini wametakiwa kukipa kipaumbele vazi la Kitenge ili kiweze kuinua viwanda vya ndani pamoja na  malighafi hiyo.

Akizungumza wakati wa Mahojiano hayo,Moja ya wabunifu wanaofanya vizuri katika utayarishaji wa vazi la Kitenge ,Irfan Riziwanali amesema Kitenge ni moja ya Malighafi inayopendwa na watu wote kutokana na rangi zake pamoja na baadhi ya michoro inayochapishwa.

"Ilinibidi nitengeneze vitu mbalimbali kama begi,nguo pamoja na viatu vikiwa na Malighafi ya Kitenge kuonyesha kwa jinsi gani nathamini viwanda vya hapa nchini pamoja na utamaduni wa Kitanzania wa vazi la Kitenge."

Hata hivyo Riziwanali ameeleza kuwa lengo lake hapo awali lilikuwa ni kutengeneza mabegi ya kipekee ambayo hapo awali hayakuwahi kubuniwa na mtu yoyote yule.

 "Ilinilazimu kushawishi Wateja kupenda bidhaa hizo na wateja walivutiwa Sana na bidhaa zetu za mabegi yaliyobuniwa na Kitenge na nitaendelea kutengeneza na kubuni vitu kwa kutumia Kitenge."

Pia amesema kupitia Sanaa hiyo ya ubunifu imeweza kumkutanisha na watu mbalimbali nje na ndani ya nchi ambao wamekua msaada katika vitu tofauti tofauti pamoja na kubadilisha mawazo kwa namna gani kazi ya ubunifu itaweza Kufika mbali.


Mbunifu hapa nchini Irfan Riziwanali akionesha Moja ya bidhaa (begi) iliyotengenezwa kwa Malighafi aina ya Kitenge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...