* LATRA CCC kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa hasa Covid-19
* Kujenga Jamii iliyostaarabika
* Kutunza vyombo vya usafiri hasa milango na madirisha
Na Mwandishi wetu
MTEJA ni mfalme hii kauli husikika zaidi kwa wafanyabiashara lakini hii inahamia kwa abiri wa Usafiri wa ardhini kwani Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini(LATRA CCC) wamedhihilisha hilo leo Septemba Mosi 2021 wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza hilo.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) ya www.latraccc.go.tz, Naibu waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amesema kuwa Baraza la LATRA CCC limedhamiria kuondoa kero za wasafiri wa Ardhini kwa kutoa elimu itakayosaidia kutoa kero hizo .
Amesema kuwa Baraza hilo teyari limeshaanza kutoa elimu ya kuwa wastaarabu wanapotumia vyombo vya moto kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwani visa vya wananchi kutumia madirisha kuingia kwenye vyombo vya usafiri zimepungua.
Hata hivyo Baraza hilo limesema kuwa Wananchi wameanza kuelekezwa kupanda mstari wanapoingia kwenye usafiri ili kupunguza baadhi ya kero zinazozuilika bila gharama yeyote.
Kwa upande wa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC, Leo Ngowi amesema kuwa baraza la LATRA CCC linampango wa kuhamasisha jamii kuingia kwenye vyombo vya usafiri kwa atakayekuwa wakwanza kufikia kituoni ndiye atakayekuwa wakwanza kupata huduma ya usafiri kistaarabu.
Hata hivyo amesema kuwa watoto, wajawazito, wazee na wagonjwa watapata huduma stahiki na kwa wakati na Kupewa kipaumbele.
Licha ya hayo kaimu katibu Mkuu wa baraza la LATRA CCC amesema kuwa wanataka kujenga jamii ambayo itakuwa na ustaarabu katika kutumia huduma ya usafiri hapa nchini pamoja na kuponya majeraha ya muda mrefu kwa abiria kwa kukaa muda mrefu vituoni.
Hivyo baraza la LATRA CCC limedhamiria kuepusha ajali na majeraha ya mwili kwa watumiaji wa usafiri wa aridhini pamoja na kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya kuambukiza hasa COVID-19.
Ngowi amesema kuwa licha ya kutoa elimu katika jamii kuwa ya kistaarabu lazima jamii iongeze utu, Umoja, upendo na Mshikamano ili kila mmoja aweze kutumia usafiri wa ardhini bila kuwa na kinyongo.
Amesema kuwa baraza la LATRA CCC wanaihimiza jamii kuanza kutumia kieletroniki katika sekta ya usafirishaji kama kutumia E-tiket kwa mabasi ya mijini na masafa marefu ili kuondoa kadhia ya wapiga debe.
Amesema watakusanya maoni kwa jamii juu ya mikinzano inayojitokeza katika sekta ya usafirishaji hapa nchini hasa kwa upande unaomwathiri mtumia huduma ya usafirishaji.
Naibu waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akifurahi mara baada ya kuzindua Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya LATRAA CCC, Dkt.George Makuke akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa LATRA CCC wakifuatilia Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC, Bw.Leo Ngowi akifuatilia hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam
Naibu waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija (waliokaa katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya LATRAA CCC, Dkt.George Makuke (wa kwanza Kushoto), Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC, Bw.Leo Ngowi (wa kwanza kulia) wakipata picha ya pamoja na watumishi wa LATRAA CCC wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa LATRA CCC wakifuatilia Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC, Bw.Leo Ngowi akifuatilia hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija (waliokaa katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya LATRAA CCC, Dkt.George Makuke (wa kwanza Kushoto), Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC, Bw.Leo Ngowi (wa kwanza kulia) wakipata picha ya pamoja na watumishi wa LATRAA CCC wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija (waliokaa katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya LATRAA CCC, Dkt.George Makuke (wa kwanza Kushoto), Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC, Bw.Leo Ngowi (wa kwanza kulia) wakipata picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Oysterbay wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija (waliokaa katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya LATRAA CCC, Dkt.George Makuke (wa kwanza Kushoto), Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC, Bw.Leo Ngowi (wa kwanza kulia) wakipata picha ya pamoja na askari wa usalama barabarani wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...