Meneja wa Tawi la Mbagala, Benki ya Biashara (TCB), Edward Moleka (kulia) akitoa maelekezo kuhusu Benki hiyo kwa Mstahiki Meya wa Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto.
Mstahiki Meya wa Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto akimlisha Keki Msimamizi Mkuu wa Matawi ya Benki ya Biashara (TCB), Tanzania Bara na Visiwani, Godfrey Nyamhanga ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Mstahiki Meya wa Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto (mwenye Suti ya kijivu) akiwa kwenye Picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya Biashara (TCB) Tawi la Mbagala katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.



Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

BENKI ya Biashara (TCB) imeaswa kusaidia huduma mbalimbali za jamii na kuinua kundi la Wanawake ili kuwasaidia kimaendeleo pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa makundi mbalimbali.


Hayo yameelezwa na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto alipotembelea Tawi la Benki hiyo, Mbagala Dar es Salaam katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.


Kumbilamoto ameipongeza Benki hiyo kusogeza huduma zake karibu na Wananchi, amesema ni wajibu kwao kuisaidia jamii ikiwemo kusaidia misaada ya Madawati ya kukalia (Desks) kwa baadhi ya Shule.


“Tutafurahi kama mtamsaidia Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika kutoa misaada ya upatikanaji wa Madawati, kwa Wanafunzi wetu na huduma nyingine za Kijamii za ujenzi wa Vituo vya afya”, amesema Kumbilamoto.

Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa Matawi ya Benki hiyo, Tanzania Bara na Visiwani, Godfrey Nyamhanga amesema wataendelea na sera yao ya kusaidia Jamii ya Watanzania ikiwa pamoja na kurudisha faida kwa Wateja katika msuala ya Elimu na Afya.


Nyamhanga amesema wataendelea kutoa kipaumbele kwa Wanawake kupitia dirisha la Wanawake katika kuwainua kiuchumi na kupata Maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...