Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula(Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Qu Dongyu. Mazungumzo hayo yamefanyika makao makuu ya shirika hilo yaliyopo Roma,Itali.

 

Dkt. Qu Dongyu ameishauri Tanzania kuchagua zao moja la kilimo miongoni mwa mazao mengi yaliyopo kwa ajili ya kuitangaza Tanzania Kimataifa na kwamba FAO iko tayari kusaidia ujuzi na kuijengea uwezo Tanzania kufikia lengo hilo .

 

Dkt. Qu Dongyu ameongeza kuwa kwa sasa FAO imeanzisha jukwaa maalum la kuwawezesha wanawake na vijana kunufaika na sekta ya kilimo kutokana na utafiti kuonesha kuwa wanawake wengi katika nchi zinazoendelea wanajihusisha na kilimo

 

Balozi Mulamula yuko Roma,Italia kushiriki Mkutano wa tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Italia pamoja na kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa amani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika nembo ya Shirika la Chakula na Kilimo duniani la Umoja wa Mataifa katika makao makuu ya shirika hilo Roma,Italia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la chakula na kilimo la kimataifa la Umoja wa Mataifa katika makao makuu ya umoja huo yaliyopo Roma,Italia


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...