*Yajipanga kutoa ushauri waondolewe ili waje wa kufanya vizuri 

Na Chalila KIbuda,Michuzi TV

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa utekelezaji wa uhamishaji wa machinga baadhi ya sehemu haujafanya vizuri kwa kuibua chuki au madhara hasi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashuri Kuu  wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa kuna baadhi ya wakuu wa mikoa na Wilaya hawajafanya vizuri hivyo watashauri kuwa hawatoshi wawekwe wengine wanaotosha wa kufanya kazi vizuri.

Amesema hadi kufikia kuzungumza hivyo wameona baadhi ya wamachinga na wafanyabiashara wadogo wameamua kufungia biashara ndani kutokana na kutojua wanakwenda wapi.

Aidha Katibu wa Itikadi na Uenezi  Halmashauri Kuu ya Chama hicho amesema kuwa viongozi waliopewa dhamana hawajashirikisha machinga kwenye kuhamisha katika maeneo yasio rasmi kwenda sehemu zenye miundombinu ya kuwezesha biashara zao kufanyika.

Shaka amesema dhamira ya Rais Samia Hassan Suluhu ni kutaka wamachinga kupelekwa sehemu zilizopangwa bila kushusha utu wake kwani ni ustaarabu ndio unahitajika.

Shaka amesema kamati za  Mikoa na Wilaya za Chama hicho zishuke na kuangalia hali ya wamachinga namna wanavyoondoka na kama kuna nguvu inatumika waweze kurekebisha kwani Chama ndo chenye dhamana na wananchi na makundi yote.

"Maagizo ya Rais Samia Hassan Suluhu yalikuwa yanataka kuwepo na ushirikishwaji wa jambo hili la machinga ili liweze kuleta matokeo chanya lakini baadhi wameshindwa kufanya hivyo"amesema Shaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...