Na Amiri Kilagalilka,Njombe


Kilimo hai au Organic farming ni aina ya kilimo ambacho huzingatia matumizi endelevu ya rasilimali za mazao ya kilimo pamoja na mifugo,Kilimo hiki hutumia mbolea isiyotengenezwa viwandani na ni aina ya kilimo ambacho huzingatia utunzaji wa mazingira.

Baadhi ya wakulima nchini wanaojishughulisha na kilimo hiki wamekuwa wakikutana na changamoto wanapohitaji kulifikia soko la mazao ya kilimo hai kutokana na kukosa elimu sahihi namna ya kukidhi vigezo vya soko hususani la kimataifa la mazao yanayotokana na kilimo hai.

Imebainika kuwa licha ya wakulima kutumia mbinu za kilimo hai na kufanya vizuri kwenye kilimo hicho lakini wamekuwa wakikubwa na changamoto kubwa ikiwemo ya utunzaji wa kumbukumbu jambo ambalo ni la msingi katika kilimo hai.

Kwa kuliona hilo bwana Valent Agligage mtaalamu kutoka shirika la kuendeleza kilimo hai Tanzania (TOAM) amekutana na wakulima wa kijiji cha Igima wilayani Wangi’ngombe mkoani Njombe wanaojishughulisha na kilimo hai kupitia asasi isiyo ya kiserikali ya NSHIDA yaani Njombe Sourthen Higland Divelopment Asociation na kutoa mafunzo ya udhibiti wa mazao ya kilomo hai ikiwa ni mkakati wa kufikia soko la mazao ya kilimo hicho.

Bwana Agligage amebainisha kuwa suala la changamoto ya soko la mazao ya kilimo hai lipo na kwa kuliona hilo serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wameendelea kushirikiana ili kuzitatua changamoto hizo na mpaka sasa Tanzania imekuwa na vikundi visivyopungua 100 vilivyokidhi vigezo na kupata uwezo wa kuuza mazao ya kilimo hai ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

“Vikundi hivi tayari vimeshapewa cheti kuuza mazao kwa kutumia alama  ya ubora kwa hiyo wana uwezo wa kuuza ndani ya Afrika Mashariki”alieleza Valent Agligage

Amesema wakulima wa kilimo hai hususani wa Parachichi mkoani Njombe wanapaswa kujua namna kutunza kumbu kumbu za kilimo chao na kuchangamkia fursa ya masoko yanapowafikia kwenye maeneo yao na hiyo itakuwa njia mojawapo ya kufikia soko.

Giliad Mwanzalila na Lucy Kilasi hawa ni baadhi tu ya wakulima wa kilimo hai cha parachichi katika kijiji cha Igima mkoani Njombe,wamesema upo umuhimu mkubwa wa kuendeleza kilimo hai kwa kuhamasishana ili kuondokana na changamoto kwa kuwa mazao ya kilimo hicho yamekuwa na faida kuwa zikiwemo za kiafya.

Nchini Tanzania kilimo hai kinawezekana,kilimo hai ni bora katika afya ya binadamu,mazingira lakini pia soko la mazao ya kilimo hicho ni kubwa ndani nan je ya nchi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...