Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo ( kulia ) akikabidhi mfano wa hundi ya sh milioni 83 kwa mshindi wa kwanza wa mauzo bora ya mbolea hiyo kwa mwaka 2020/2021, Mkurugenzi wa Ngelela Agrovet Company Ltd, Boniphace Ngelela wakati wa mkutano mkuu wa kila mwaka wa mawakala na washirika wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Tanzania ( TFRA), Dk. Stephan Ngailo na Meneja kutoka kampuni ya Ngelela, Mussa Ngelela.



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo ( kulia ) akikabidhi mfano wa hundi ya sh milioni 57 kwa mshindi wa pili wa mauzo bora ya mbolea hiyo kwa mwaka 2020/2021, Mkurugenzi wa Ng`wana Igwembe Agrovet Company Ltd, Yahya Bundala na Mkewe, Hamisa Sagata wakati wa mkutano wa kila mwaka wa mawakala na washirika wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Tanzania ( TFRA), Dk. Stephan Ngailo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo ( kulia ) akikabidhi mfano wa hundi ya sh milioni 54 kwa mshindi wa tatu wa mauzo bora ya mbolea hiyo ya mwaka, Mkurugenzi Msaidizi wa Mtewele General Traders, Deogratius Mtewele wakati wa mkutano mkuu wa kila mwaka wa mawakala na washirika wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA), Dk. Stephan Ngailo.

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Mbolea ya Yara, Sheilla Chato akizungumza na mawakala na washirika wa kampuni hiyo katika mkutano mkuu wa kila mwaka kutoka mikoa mbalimbali nchini uliondaliwa na kampuni hiyo na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Tanzania ( TFRA), Dk. Stephan Ngailo ( kushoto) akikabidhi cheti cha ushirikiano bora kwa Mkurugenzi wa Biz Agrovet, Masoud Salim Nassor kutoka Zanzibar, wakati wa mkutano mkuu wa kila mwaka wa mawakala na washirika wa Kampuni ya Mbolea ya Yara kutoka mikoa mbalimbali nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo.

Baadhi ya wakala na washirika wa Kampuni ya mbolea ya Kampuni ya Yara wakihudhuria mkutano mkuu wa kila mwaka wa wakala hao kutoka mikoa mbalimbali nchini uliondaliwa na kampuni hiyo na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

Bwanashamba Mwandamizi Mstaafu wa Kampuni ya Mbolea ya Yara, Maulidi Mkima akizungumza katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo akizungumza na mawakala na washirika wa Kampuni ya Mbolea ya Yara kutoka mikoa mbalimbali nchini katika mkutano mkuu wa kila mwaka uliondaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Deogratius Mtei akizungumza katika hafla hiyo.



Wafanyakazi wa kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata vyeti cha utumishi wa muda mrefu wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na kampuni hiyo baada ya mkutano mkuu wa kila mwaka wa mawakala na washirika wa kampuni yao kutoka mikoa mbalimbali nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo ( kulia), wafanyakazi wa Yara, mawakala na washirika wa kampuni ya Yara wakiselebuka, katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na kampuni hiyo baada ya mkutano mkuu wa kila mwaka wa mawakala na washirika wa Yara kutoka mikoa mbalimbali nchini jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo ( kushoto) akimpongeza Mkurugenzi wa Biz Agrovet, Masoud Salim Nassor kutoka Zanzibar, baada ya kuibuka kidedea katika droo iliyochezwa na kushinda safari ya kwenda katika muga za wantama za Ngorongoro na Serengeti kwa siku nne wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na kampuni hiyo baada ya mkutano mkuu wa kila mwaka wa mawakala na washirika wa mbolea ya kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Tanzania ( TFRA), Dkt. Stephan Ngailo ( kushoto kwa Bwana Odhiambo) wakiwa katika picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Yara, mawakala na washirika wa kampuni hiyo mara baada ya kumalizima kwa mkutano mkuu wa kila mwaka kutoka mikoa mbalimbali nchini jijini Dar es Salaam jana. .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...