Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MBUNGE
wa Jimbo la Kibaha Mjini,Silvestry Koka , ametoa rai kwa mamlaka ya
maji safi na usafi wa mazingira ( DAWASA), kuangalia mfumo rahisi wa
kuunganishia wananchi huduma ya maji safi katika kata ya Mbwawa,ili
kupunguza gharama kubwa ya usambazaji maji.
Ameeleza
hatua hii itawezesha malengo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kumtua
ndoo mama kichwani kufanikisha pasipo kuweka gharama kubwa zinazowabana
watumiaji ambao wengi wao wana uwezo duni .
Koka
alitoa rai hiyo katika ziara yake kata ya Mbwawa, ambapo alipokea
malalamiko ya mradi wa maji Mlandizi-Mbwawa unajengwa kwa bilioni 1.1
ambao bado hautoi maji ya uhakika licha ya kuwa kwenye hatua ya
usambazaji kwa wateja.
Kufuatia
kero hiyo ,mbunge huyo ameunda kamati itakayoanza kazi mara moja
kufuatilia changamoto hizo kwa meneja DAWASA na ikishindikana kufika kwa
mkurugenzi mtendaji ili kupata ufumbuzi .
"Dhamira
ya serikali ya awamu ya sita chini yake Samia Suluhu Hassan ni kuona
miradi ya maji inaleta matokeo na tija kwa wananchi ,Itakuwa ni mchezo
kama miradi inayogharimu fedha nyingi kukamilika pasipo wananchi
kunufaika nayo "alifafanua Koka.
Aidha
Koka aliwaagiza watendaji wa kata na maeneo ya pembezoni, wasiwe chanzo
Cha migogoro ya wakulima na wafugaji na kuwataka wachukue hatua kuondoa
kero hiyo kandamizi kwa wakulima.
Pamoja
na hayo ,alisema anaendelea kupigania barabara kwa kiwango cha lami
Mlandizi -Makofia ili fedha itoke na kuanza ujenzi ,na kuongeza ni
barabara ambayo ipo katika utekelezaji wa ilani hivyo wananchi wavute
subira.
Koka
alieleza ,kwasasa lengo lake ni kuona kata za pembezoni ikiwemo Mbwawa
inasogezewa huduma za kijamii kwa kasi kama shule za
sekondari,vyuo,vituo vya polisi ,maji na umeme kama ilivyo kata zilizopo
mjini .
Katika
hatua nyingine Koka aliwaasa ,wananchi kulinda mali na miundombinu ya
miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na maji na kuacha udokozi kwani
kunakwamisha utekelezaji wa miradi .
Akijibu
kuhusiana na changamoto za mradi wa maji, mwakilishi kutoka DAWASA
,Yohana alisema suala hilo lipo ndani ya uwezo wa meneja DAWASA.
Alisema pia tatizo la kupasuka kwa mabomba chakavu yaliyo katika mtandao wa zamani linashughulikiwa ili kupata maji ya uhakika .
"Mbwawa
ilikuwa haina maji ,tulianza na wateja 159 hadi Mbwawa Miswe kuwaingiza
kwenye mtandao wa zamani walikuwa wanapata maji Bagamoyo,Ila chanzo Cha
Bagamoyo hakikidhi Cha Mlandizi ndicho cha uhakika"alieleza Yohana.
Awali
diwani wa kata ya Mbwawa Judith Mluge alisema, wanakabiliwa na
changamoto ya mabomba kupasuka mara kwa mara hali inayosababisha kukosa
maji ,ukosefu wa shule ya sekondari.
Wakazi
wa Mbwawa Asha Matambo,Mzee Shomali walibainisha ,wanatakiwa kulipia
gharama za kuunganishiwa maji sh.200,000- 800,000 kwa umbali wa mita
tano kiasi ambacho ni kikubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...