Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WANAFUNZI
wanaosoma elimu ya sekondari wanapata kero ya kwenda kufuata elimu ya
sekondari eneo jirani la Miembe Saba ,umbali wa km 15 kwenda na kurudi
km 30 hali ambayo inasababisha baadhi ya wanafunzi kujiingiza kwenye
makundi yasiyo na maadili .
Aidha wanafunzi hao hupata shida ya kutumia bodaboda sh.6,000 kwenda na kurudi na wengine wasio na uwezo kutembea kwa miguu.
Hayo
yalijiri katika mkutano wa hadhara katika ziara ya mbunge ukagua wa
Jimbo la mji wa Kibaha ,Silvestry Koka kwenye kata ya Viziwaziwa ambapo
alianzia kukagua eneo la ujenzi wa shule ya msingi Sagale Magengeni
lenye heka nne na kugharimu milioni 17 na kukagua ujenzi wa vyumba
vitatu shule ya sekondari kata ya Viziwaziwa iliyogharimu zaidi ya
milioni 58.
Akitoa
kero hiyo diwani wa kata ya Viziwaziwa ,Mohammed Chamba alisema
wanafunzi hao wanapata shida hivyo shule hiyo ya sekondari ikikamilika
itakuwa mkombozi.
Chamba
alieleza,pia kuna Changamoto ya ukosefu wa umeme Sagale Magengeni,
tatizo la malipo ya mfumo wa kusambaziwa maji na ukosefu wa kituo Cha
polisi.
"Zahanati Changamoto kubwa ya watumishi na ukosefu wa chumba Cha wakimama kujifungulia na mashamba pori yaliyokithiri"alieleza.
Nae Koka alisema ,mkakati wake ni kupigania kupeleka maendeleo na huduma za jamii katika kata za pembezoni.
Katika
elimu Koka alisema ,wamejenga shule ya sekondari kwa nguvu za wananchi
katika ujenzi huu alikuwa kipaombele na kuchangia milioni nne na kutoa
milioni mbili kwa ajili ya choo japo kinahitaji kuboreshwa.
Alisema, Shule hii ianze haraka kabla ya lengo la kupangwa kuanza mapema mwakani .
Koka
alisema shule ya msingi Sagale Magengeni kumepatikana eneo la shule
ambapo bado inahitajika milioni saba ,"mbunge huyo atachangia milioni
mbili ili kuanza ujenzi .
Katika
afya kwenye zahanati ya Viziwaziwa mpango uliopo ni kuona maeneo ya
pembezoni kunapatikana vituo vya afya ikiwemo kutanua zahanati hiyo.
Kwa
upande wa wakazi wa kata ya Viziwaziwa,akiwemo Rich Shayo na
Christopher Ngonyani walisema elimu ya sekondari iharakishwe ili
kukomboa wanafunzi wanaosumbuka kwasasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...