Na Amiri Kilagalila,Njombe
Katika
kuadhimisha siku ya kimataifa ya wazee duniani waandishi wa habari
wanawake mkoani Njombe wamepongezwa kwa kuandaa hafla fupi
iliyowakutanisha baadhi ya wazee na kusheherekea nao pamoja na
kuhamasisha zoezi la chanjo ya Uviko 19
Akizungumza
kwenye halfa hiyo ambayo imefanyika katika ukumbi wa Turbo mjini Njombe
mgeni wa heshima ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wanawake
wa Chama cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Njombe Beatrice Malekela amesema
jamii inatakiwa kuwakumbuka wazee kwa kuwasaidia mahitaji muhimu kama
ambavyo kundi la wanahabari wanawake mkoa wa Njombe lilivyofanya.
"Pia
serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imeweza kuwatambua wazee wa
mikoa yote ambapo kwa mkoa wa Njombe tuna wazee 39,768 na kwa kweli
niwapongeze sana waandishi wa habari kwa hiki mlichokifanya kwani
mmeiunga mkono serikali katika juhudi za kuwasaidia wazee"alisema
Betrice Malekela
Aidha
Betrice amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inathamini
uwepo wa wazee kwenye jamii ambapo imewapa kipaumbele katika kupata za
huduma za afya kwa kuwapatia vitambulisho vinavyowasaidia kupata
matibabu bure.
Sophia
Issa ni mwenyekiti wa muda wa umoja wa waandishi wa habari wanawake
mkoa wa Njombe amesema watahakikisha wanaendelea kuandika habari zenye
kuwakumbusha watanzania wafahamu umuhimu wa wazee na kuondoa dhana
potofu juu yao.
"Wanahabari
tumekuwa tukifanya kazi nyingi huko vijijini zinazohusu wazee na
changamoto zao ikiwemo za kutelekezwa.Tunaendelea kuhamasisha watoto
walioenda mijini na kuwaacha wazee vijijini waweze kuwakumbuka
wazazi,babu na bibi zao" alisema Sophia Issa
Kwa
upande wa baadhi ya wazee waliohudhuria hafla hiyo wamewashukuru
wanahabari wanawake kwa kuwajali huku pia wakiowaomba baadhi ya vijana
wawakumbuke wazee na kuwatunza.
"Kwa
serikali tunashukuru kwa huduma ya afya,Mimi mwenyewe natibiwa bure na
pia niwaombe vijana wasitunyanyapae sisi wazee"alisema mmoja wa wazee
Waandishi hao wanawake wa mkoa wa Njombe wamekabidhi zawadi mbali mbali kwa wazee ikiwemo Sukari,sabuni na mafuta ya kupikia
Maadhimisho
ya siku ya kimataifa ya wazee Duniani yanayoadhimishwa leo Octoba
1,2021 yameambatana na kauli mbiu isemayo "Matumizi sahihi ya kidigitali
kwa ustawi wa rika zote".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...