NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO
Mjumbe wa chama cha mpira wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma bwana Issa Likokwe mkazi wa mamlaka yamji mdogo wa Lusewa , amenusurika kifo baada ya kupokea kipigo kutoka kwa mashabiki wa timu ya Madridi ya mtaa wa Milonji katika mamlaka ya mji mdogo huo.
Akisimulia mkasa huo Likokwe alisema alikutwa na mkasa wa kushambuliwa kimwili na mashabiki 17 wa timu ya Madridi ya mtaa wa milonji siku ya fainali ya timu hiyo na timu ya Sungura siku ya jumapili wiki iliyopita ambapo alipigwa magongo kichwani na ubavuni.
Aidha Likokwe alidai chanzo cha tatizo hilo lilikuwa timu ya Madridi ilikata rufaa kuilalamikia timu ya Sungura kuchezesha wachezaji Zaidi ya sita kutoka nje ya Kijiji badala ya wachezaji watano kadiri ya kanuni ya ligi hiyo .
Bwana Likokwe alisema malalamiko hayo yalionekana hayana msingi wowote na kuwataka timu ya Madridi kuingia katika mechi ya kumtafuta bingwa wa ligi hiyo kati ya timu hiyo na timu ya Madridi ambapo siku ya fainali timu ya Sungura iliingia uwanjani na timu ya Madridi haikuingia uwanjani hali iliyomfanya msimamizi wa ligi hiyo bwana Likokwe awape ushindi wa pointi tatu na magori mawili timu ya Sungura na kuibua hasira kwa mashabiki wa timu ya Madridi na kumshushia kipigo na kuzimia.
Kaimu mtendaji wa mtaa wa milonji bwana Iddi Majidu Pilly alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa ofisi ya mtaa iliandika barua ya kusimamisha ligi hiyo baada ya kubaini viashiria vya uvunjifu wa amani wakati wa uendeshaji wa ligi hiyo lakini mwendesha ligi aliendelea mpaka siku ya fainali na kutokea kilichotokea alisema Pilly.
Pilly aliongeza kuwa ofisi yake ilijaribu kutuliza ghasia za mashabiki na kumfikisha msimamizi wa ligi hiyo kituo cha afya Lusewa baada ya kushambuliwa na mashabiki wenye hasira kwa kupigwa magongo kichwani na ubavuni.
Mganga mkuu wa kituo cha afya Lusewa peter Ndunguru alikiri kumpokea na kumpatia matibabu bwana Issa Likokwe kwa kumtibu majeraha aliyoyapata wakati anapigwa na mashabiki hao wa timu ya Madridi na kudai kuwa afya ya bwana Likokwe inaendelea kuimarika baada ya kupata matibabu hayo.
Mwenyekiti wa chama cha mpira wilaya ya Namtumbo NADIFA bwana Zuberi Kossa Pamoja na kusikitishwa na tukio hilo alisema amemtaka bwana Likokwe kuandika barua kwenye chama cha mpira akilalamikia kitendo hicho ili chama pamoja na mambo mengine kiweze kuchukua hatua za kisheria kwa timu zenye mashabiki wa tabia za kujichukulia sheria mkononi kwani hawakuwa na sababu ya kumpiga msimamizi lakini walitakiwa kucheza fainali hiyo na kukata rufaa yao kwa kutoridhishwa na timu pinzani kuchezesha wachezaji Zaidi ya sita kutoka nje ya Kijiji chao.
Timu zilizoshiriki ligi hiyo zilikuwa timu 8 ikiwemo ya Sungura, Chelsea,Madridi,Small boys,Boss Mtoto ,Azam ,matha mtoto, na timu ya Kbc zote za mtaa wa milonji katika mamlaka yam ji mdogo wa Lusewa na timu ya Sungura kuchukua ubingwa ligi hiyo na kusababisha vurugu ya kipigo cha msimamizi wa ligi hiyo wakati wa kugawa zawadi kwa washindi wa ligi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...