Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
WAZAZI na walezi wanatakiwa kuwasaidia Mabinti wanaopevuka katika kuhakikisha wanapata hedhi salama na vifaa vya kujikingia ipasavyo (Taulo za kike)bila kuwajengea hofu au aibu pindi wanapokuwa kwenye siku zao.
Akizungumza na Michuzi Tv, Mkurugenzi wa Kampuni ya Taulo za kike (Nice and free ) Nice Kennedy Mamuya amesema Wazazi pamoja na Walezi wanajukumu la kuhakikisha Mabinti wanapatiwa Elimu ya hedhi salama na kuwajengea uwezo wa kutokuona kuwa kwenye siku zao ni kitendo c upha aibu au kukosa kujiamini mbele za watu na hata Mashuleni.
"Walezi au Wazazi wakishirikiana vizuri na watoto wao inaweza ikamjengea uwezo Binti katika kukabiliana na hedhi salama na kuvunja taswira iliyojengeka kwenye jamii kuwa Hedhi ni kitendo cha aibu au jambo la kificho"
Hata hivyo ameeleza kwa namna gani Kampuni hiyo iko bega kwa bega kushirikiana na jamii hasa Mashuleni kutoa Taulo kwa watoto wasioweza kujikimu kununua Taulo .
"Tumeguswa kushirikiana na "Nakupenda Marathon" tumeweza kuchangia Taulo za kike zipatazo 500 kwa ajili ya Kusaidia Wasichana Mashuleni katika visiwa vya Zanzibar kuweza kujikimu na jambo hili litakua endelevu kwa Mashule mbalimbali nchini.
Pia amesema taulo hizo ni salama na zilizotengenezwa kwa pamba asilimia 100 zenye uwezo wa kufyonza uchafu wote na kumuweka huru mtumiaji .
Na amewataka vijana wanaotafuta ajira waweze kutumia fursa hiyo kama sehemu ya uwakala wa kusambaza taulo za kike aina ya Nice madukani kwa upande wa Visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Taulo za kike (Nice and free) Nice Kennedy Mamuya akikabidhi 'box' la Taulo za kike kwa Muwakilishi wa "Nakupenda Marathon " kama sehemu ya Kuchangia Mabinti Mashuleni kukabiliana na hedhi salama
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...