Maafisa wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakibandika stika ya usajili wa magari yanayotoa huduma ya majitaka baada ya kumaliza zoezi hilo  litakalodumu kwa muda wa siku 14 kuanzia Oktoba 1 hadi 16 mwaka huu

Afisa Biashara wa Mabwawa ya Majitaka DAWASA Mwajuma Hamza (katikati) akiendelea na zoezi la usajili kwa wamiliki wa magari yanayotoa huduma ya majitaka linaloendeshwa na Mamlaka hiyo lililoanza Oktoba 1 mwaka huu na litadumu kwa muda wa siku 14.

 

Afisa wa  DAWASA akimkabidhi stika mmoja wa wamiliki wa magari ya majitaka baada ya kumaliza zoezi la Usajili wa magari hayo linaloendeshwa kwa siku 14  katika eneo la Vingunguti.


**********************************


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) limewataka wamiliki wa magari  binafsi yanayotoa huduma za majitaka kujitokeza kwa ajili ya zoezi la utambuzi na utoaji huduma ya utoaji majitaka kwa Wananchi.

Hayo yamesemwa na Afisa Biashara DAWASA, Mwajuma Hamza wakati wa zoezi hilo lilioambatana na utoaji wa vibali vya utoaji huduma ya majitaka kwa waendeshaji binanfsi wa huduma hiyo.

Mwajuma amesema, lengo la zoezi hilo ni kuratibu huduma ya majitaka kupitia magari binafsi na kuhakikisha kuwa majitaka yanayonyonywa kutoka sehemu mbalimbali ndani ya eneo la kihuduma DAWASA yanamwagwa kwenye  mabwawa ya majitaka yanayomilikiwa na DAWASA na sio vinginevyo.

“Zoezi hili linafanyika katika Mabwawa ya majitaka Vingunguti ambapo magari yatakayosajiliwa yatabandikwa stika za DAWASA na kupewa cheti cha kukubaliwa kutoa huduma baada ya kuwa amedhibitishwa na Mamlaka.”amesema Mwajuma

“Tunafanya usajili huu kila mwaka na lengo ni kupata takwimu sahihi ya watu tunaofanya nao kazi  kila siku na baada ya usajili gari ambalo halina usajili halitaruhusiwa kumwaga majitaka kwenye mabwawa ya DAWASA,”

Aidha, Mwajuma amesema DAWASA inaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi majitaka na maji yanayochukuliwa kutoka majumbani yanakuja kwenye mabwawa na yanatibiwa kwa ajili ya matumizi mingine.

Mwajuma amesema, mwitikio wa usajili umeanza vizuri na mwaka huu utaratibu wa usajili ni bure kwa magari yote na mmiliki anatakiwa kufika na vitu kadhaa ikiwemo picha 2 za rangi, kitambulisho cha Kupigia kura au cha Taifa, nakala ya kadi ya gari, bima ya gari na nakala ya leseni ya Dereva vilivyothibitishwa na mwanasheria.

Zoezi hilo la usajili litadumu kwa siku 14 kuanzia octoba 1- hadi Octoba 16 mwaka huu na litaendeshwa katika mabwawa ya majitaka Vingunguti

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...