Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi amefunga Semina ya 23 'Research Workshop' iliyokuwa na lengo la kutoa mafunzo maalumu ya kuwandaa wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti kabla ya kuhitimu mafunzo kutoka bodi hiyo yaliyoanza Sepitemba 27 hadi leo Oktoba 01, 2021.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Godfrey Mbanyi amesema wanafunzi wa Bodi wanapaswa kuwa waaminifu kwenye sehemu za kazi ili serikali iweze kupata kodi stahiki ili kufikia malengo yaliyowekwa hasa kuhudumia wananchi.
Mbanyi amesema, serikali iko macho na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wale wanaokiuka maadali ya Taaluma ya Ununuzi na Ugavi. Pia amesisitiza wale anaokuwa wazoefu kazini inahitaji sana kuwalea wafanyakazi wachanga au waajiliwa wapya wawe na maadili mazuri hasa kwenye kufanya kazi za manunuzi.
Aidha amewakemea vikali watu ambao ni wazoefu kazini kuwaelekeza waajiliwa wapya kwenye maeneo ya kazi taratibu na njia mbaya zinazokiuka mienendo na maadili ya taaluma ya ununuzi na ugavi.
Pia amesema hii itaweza kusaidia kutoa huduma nzuri kwa wananchi na kuondoa lawama ambazo zinaweza kutolewa kwa Serikali. Na Serikali pia inaweza kulaumiwa na matendo ambayo yanatendwa na watendaji ambao wameaminiwa kuweza kufanya kazi kwa niaba ya hao wananchi.
Leo baada ya kuhitimu mafunzo ya siku tano wahitimu wamepewa vyeti vya kuonesha ushiriki wao katika mafunzo hayo ili kuanza kuandika research proposal/ mapendekezo ya tafiti zenu mapema iwezekanavyo.
Wanafunzi wa Bodi wapatao 134 wameshiriki mafunzo maalumu ya kuwandaa wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti kabla ya kuhitimu mafunzo yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi akiwakabidhi baadhi ya wanafunzi wa Bodi walioudhulia semina ya 23 'Research Workshop' iliyokuwa na lengo la kutoa mafunzo maalumu ya kuwandaa wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti kabla ya kuhitimu mafunzo kutoka bodi hiyo.
That's cool
ReplyDelete