WAZIRI wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda, ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kuendelea kutoa mchango wake kwa maendeleo and ukuaji wa za zao la kahawa hapa nchini.
“Ninatambua mchango wa TADB kwa maendeleo na ustawi wa zao la kahawa hapa nchini na ushiriki wenu kwenye Maonyesho ya Kahawa Mwaka 2021 yanayofanyika hapa mjini Moshi ni kielelezo tosha cha dhamira yenu,” alisema Waziri Mkenda.
Benki ya TADB imetoa jumla ya Bilioni 130.81 kwenye zao la kahawa kwa wakulima nchini, ambayo inajumuisha viatilifu, mashine za kahawa, mbolea, vituo vya CPU, ujenzi wa maghala, na uoteshaji wa miche Ngara.
Akizindua Tamasha la Kahawa sambamba na kusherekea Siku ya Kahawa Dunia zinazosherekewa kitaifa mkoani Kilimanjoro mwisho mwa wiki, Waziri Mkenda alisema, “Nimeona mambo mengi katika maonyesho haya ikiwemo, Miche bora, ufungaji wa kahawa umekua mzuri sana, na Nashukuru kwa Mabenki yetu hususani Benki yetu ya maendeleo ya kilimo (TADB) kwa kudhamini na kushiriki Tamasha hili na muendelee kuwagusa wakulima wa kahawa moja kwa moja.”
Waziri Mkenda alisemaTanzania kwa Afrika mashariki ndio nchi pekee tunaozalisha Kahawa ya papo hapo (Instant Coffee). Hivyo kuna kaza kubwa yakuendelea kuitangaza kahawa ya Tanzania ili kuweza kufungua masoko zaidi Afrika.”
“Nimeongea na TADB na wameonyesha utayari wa kutoa fedha kwa wakulima ili kubadilisha miche yao yenye tija kubwa ili kuongeza uzalishaji wa kahawa nchini,” alisemaProfesa. Adolf Mkenda.
Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Maendeleo ya Biashara, Bw. Zakayo Mphuru ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw Frank Nyabundege alisema ushiriki wa TADB kweye maonyesho ni kutambua mchango wa mnyororo wa thamani wa zao la kahawa hapa nchini.
”Sisi kama TADB tunashiriki haya maonyesho ya siku ya kahawa duniani kwasababu TADB imekua mdau mkubwa wa mnyororo mzima wa thamani wa zao la Kahawa na kimsingi naTADB imehusika moja kwa moja kuwezesha sekta hii kukua kwa kuwafikia zaidi ya wakulima wanufaika 150,000 wa zao la kahawa,” alisema.
Tamasha hilo la Kahawa lililofunguliwa na Waziri Mkenda lilihimishwa kwenye kiwanja cha Uhuru Park mjini Moshi jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...