Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali (AG) Dkt Eliezer Feleshi
amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, kwa kumuamini na
kumteua katika nafasi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali.
Dkt Feleshi ametoa shukrani hizo leo( Alhamisi) Jijini
Dodoma, akisimama kwa mara ya
kwanza mbele ya Bunge hilo tangu alipoteuliwa kuwa AG na baada ya kula
kuiapo cha uaminifu kwa Bunge hilo, wakati alipokuwa akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
mbalimbali ( Na 6) wa mwaka 2021 katika Mkutano wa Tano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Napenda kuchukua
fursa hii kumshukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muugano
wa Tanzania kwa kuniamini na
kuniteua katika nafasi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali.” Akasema AG Feleshi
Na kuongeza “
Ninamuahidi kutekeleza majukumu yangu
haya mapya kwa weledi, umahiri na
uamininifu mkubwa”.
“Pili nimshukuru Mungu tena kwa kuniwezesha kusimama kwa mara ya kwamba mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Na 6) wa
Mwaka 2021” akasema Mhe. Mwanasheria
Mkuu wa Serikali.
Akiwasilisha Muswada huo wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali
( Na 6) wa mwaka 2021 ( The Written Laws
( Miscelaneous Amendiments) No (6), Bill.2021, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Muswada huo unapendekeza marekebisho katika
sheria zifuatazao;
Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332; Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438 na Sheria
ya Kodi la Ongezeko la Thamani, Sura ya
148.
Kwa mujibu wa AG Feleshi, Muswada aliouwalisha mbele ya
Bunge, umegawanyika katika sehemu Nne ambapo sehemu ya kwanza ya Muswada
inaainisha masharti ya utagulizi, ikiwa
ni pamoja na jina la Sheria pendekezwa na tamko la marekebisho ya sheria
mbalimbali zinazokusudiwa kufanyiwa marekebisho kupitia Muswada huo.
Akalieleza Bunge hilo kwamba, sehemu ya pili ya Muswada huo inapendekeza
marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332, ambapo
kifungu cha 83B kinapendekeza
kufutwa kwa lengo la kuondoa kodi ya
zuio ya asilimia mbili kwa mazao
ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
“Lengo la marekebisho ya haya ni kulinda vipato vya wakulima kwa kuwapunguzia
mzigo unaotokana na utozwaji wa kodi” amebainisha Dkt. Feleshi.
Kuhusu sehemu ya tatu ya Muswada, ikisomwa pamoja na Jedwali
la marekebishoa ya Serikali ,
inapendekeza marekebisho katika Sheria ya Usimamizi wa kodi Sura ya 438 ili
kurekebisha kifungu cha 7 kwa kuongeza
kufungu kidogo cha 3.
“Marekebisho hayo
yanalenga kutambua Mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini
Uganda kwenda Chongoleani Tanga ili utekelezaji wa sheria za kodi usiathiri masharti mahususi ya
mkataba huo kama ilivyokubaliwa na pande zote
Kuhusu sehemu ya Nne
ya Muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, upande wa sehemu ya Nne ya Muswada inayopendekeza marekebisho ya
kufuta sheria ya kodi ya ongezeko la
thamani Sura ya 148, inapendeleza kufutwa. “ Hatua hiyo inatokana na mashauriano ya kina
kati ya Serikali na Kamati
WAKATI HUO HU, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Feleshi, amewapongeza watumishi wote wa
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Dkt, Evaristo Longopa kwa kuendelea kutekeleza majukumu na kazi za Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
ikiwamo kuandaa Muswada huo na ambao umesimamiwa kwa karibu na Bw, Onorius Njole, Mwandishi Mkuu wa Sheria akishirikiana na Waandishi wa
Sheria wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
“ Tunatambua na tutaendelea kutekeleza majukumu yetu kwa weledi, ufanisi na kuweka mbele maslahi ya nchi yetu”
amesisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Feleshi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...