Kampuni ya simu za mkononi Airtel imeingia ubia na na kampuni inayotoa huduma za usafiri wa anga nchni PrecisionAir kwa kuzindua promosheni mpya itakayowawezesha wateja wake nchini kufurahia punguzo la asilimia tano kwa wateja wote watakaolipia tiketi za kusafiri na PrecisionAir kupitia Airtel Money.
Airtel
Money na PrecisionAir wametangaza kuanza kwa promosheni hiyo maalum leo
ambapo utawapatia wateja wa Precision Air urahisi katika kupanga safari
zao na kuwawezesha kununua ticket zao wakati wowote kupitia huduma ya
Airtel Money.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa
Airtem Money Bw, Isack Nchunda alisema "ushirikiano wetu tunaotangaza
leo utawaongezea wateja wetu wa Airtel urahisi na uhakika wakati wa
kulipia safari zao za ndani na za nje kwa kufanya malipo kidigitali
pale wanapohitaji tiketi wakiwa popote .
“kupitia ofa hii mpya
sasa wateja wetu wataweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege
kupitia huduma ya Airtel Money kisha mteja atapata punguzo la asilimia
tano ya pesa aliyolipia tiketi hiyo. “ujio wa makubaliano haya
unadhihirisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora za malipo kidigitali
huku tukiwahakikishia wateja unafuu zaidi kwa kuwarejeshea kiasi cha
pesa hizo ili wazitumie kufanya mambo yao mengine”. Aliongeza Nchunda
Akiongelea
kuhusu ushirikiano huo Mkuu wa Biashara wa Precision Air Bi Lilian
Mremi alisema “ushirikiano huu umekuwa wakati muafaka ambapo Precision
Air ikiwa imejipanga zaidi kuwahudumia wateja kwa nakufanya huduma za
usafiri wa anga kuwa zakipekee
“Wateja wetu sasa wanaweza
kufanya malipo ya tiketi zao za ndege kupitia huduma ya Airtel Money.
Hii maana yake ni kujihudumia mwenyewe kupitia simu yako ya mkononi,
mteja unaweza kutembelea tovuti yetu XXXXX kufanya booking ya safari
kisha akalipia kupitia Airtel Money na kupokea tiketi yake ya
kielectroniki kupitia simu yake ya mkononi” aliongeza Mremi
Akiongea
kuhusu namna ya kupata huduma hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando alisema” huduma hii ni rahisi kutumia , mteja anachotakiwa
kufanya ni kufanya booking ya safari au kufanya booking kupitia tovuti
ya Precision Air ambapo mteja atapewa namba ambayo itatumika kama
kumbukumbu/ reference wakati wa malipo. Kununua tiketi kupitia Airtel
Money wateja wanatakiwa kufanya yafuatayo Piga *150*60#
Chagua namba 5 (Lipia bili)
Chagua namba 2 (Chagua kampuni)
Chagua namba 3 (Usafiri wa anga)
Chagua namba 2 (PrecisionAir)
Ingiza Kiasi cha pesa
Ingiza namba ya Kumbukumbu-(booking number)
Vilevile
ipo njia nyingine mteja anaweza kuitumia kwa kuingia kwenye My
AirtelApp na kufuata utaratibu huo. Mara baada ya mteja kufanya hayo
atapokea ujumbe wenye uthibitisho wa malipo na tiketi yake “aliongeza
Mmbando.
Jinsi ya kununua tiketi yenye punguzo
• Tembelea tovuto ya PresisionAir
• Chagua ndege na tarehe ya safari yako
• Chugua namba ya siti
• Ingiza namba yako ya offa/ ATLPW
• Pata kiasi kamili cha punguzo
• Lipa kupitia Airtel Money
Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda (kushoto) na Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Lillian Masawe wakionyesha bango baada ya kutangaza ushirikiano mpya ambapo kuanzia sasa wateja wa Airtel watakuwa wanapata punguzo la hadi asilimia 5 pale wanapolipia tiketi kwa kupitia huduma wa Airtel Money.
Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza ushirikiano baina ya Airtel Tanzania na Precision Air ambapo kwa sasa wateja watapata punguzo la hadi asilimia tano wanapolipia tiketi kwa kupitia Airtel Money. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Lillian Masawe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...