Benki ya Exim imetangaza washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’inayoendeshwa na benki hiyo ikilenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana huku wakipata fursa za kunyakua zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu pamoja na gari aina Toyota Vanguard.
Akitangaza
washindi wa droo ya kwanza ya kampeni hiyo iliyofanyika leo jijini Dar
es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano Msaidizi wa Benki hiyo Bi
Mariam Mwapinga alisema jumla ya washindi 6 walipatikana kupitia droo
hiyo na kujishindia zawadi ya shillingi million sita fedha taslimu.
“Katika
droo ya leo jumla ya washindi sita (6) wamepatikana na wameweza
kujishindia zawadi za fedha taslimu kiasi cha sh mil 6. Washindi hawa
sita watakabidhiwa zawadi zao katika maeneo yao waliopo na tutaendelea
na droo kama hizi kila mwezi na washindi wataendelea kuingia kwenye droo
itakayowawezesha kushinda zawadi kubwa ya gari aina ya Toyota
Vanguard.’’
“Wateja wetu wa sasa na wale wapya watakuwa kwenye
nafasi ya kujishindia zawadi hizi kila wakapojiwekea akiba ya kuanzi
Tsh. 500,000 na kuendelea. Kadili wanavyojiwekea amana kubwa zaidi
ndivyo wanavyojiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi kubwa zaidi,’’
alisema Bi Mariam wakati wa droo hiyo iliyohudhuriwa pia na muwakilishi
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini.
Akifafanua zaidi
kuhusu kampeni hiyo Bi Mariam alisema inalenga kuleta mabadiliko kwenye
mtazamo wa uhifadhi wa amana miongoni mwa watanzania kutoka kuhifadhi
pesa majumbani na badala yake wazihifadhi kupitia benki hiyo kwa usalama
wa fedha zao sambamba na faida nyingine nyingi ikiwemo riba.
“Lengo
si tu kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea amana,
tunachohitaji ni kuona kwamba Watanzania wengi wanajiwekea amana zao
sehemu salama ili kujiendeleza kukua kiuchumi ndio maana tumejipanga
kuwahamasisha watumie akaunti zetu mbalimbali ikiwemo akaunti ya
mshahara inayotumika kwa matumizi mbalimbali ya kila siku,’’ alitaja.
Alitaja
akaunti nyingine kuwa ni pamoja na akaunti ya mzalendo inayoendeshwa
bila makato ya kila mwezi, akaunti ya haba na haba, akaunti ya faida
ambayo inakuruhusu kuweka akiba na kupata riba pamoja na akaunti ya
Nyota ambayo ni akaunti maalum kwa ajili ya Watoto pamoja na akaunti ya
wajasiriamali inayowahudumia wafanyabiashara na mahitaji yao tofauti
tofauti ya kibiashara.
Kwa upande wake Ofisa kutoka Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Bi Bi Neema Tatock alitoa pongezi kwa washindi wa
promosheni hiyo huku akiwahamasisha walengwa kushiriki kwa wingi na
kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo
zinazofuata huku akiwahakikishia kuwa Bodi hiyo imejipanga kuhakikisha
zoezi la kupata washindi linafanyika kwa kwa uwazi na kwa kufuata
misingi halali ya kubahatisha.
Meneja Masoko na Mawasiliano Msaidizi wa Benki ya Exim Bi Mariamu Mwapinga (wa kwanza kushoto) akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani ) zawadi kubwa ya gari aina ya Toyota Vanguard itakayotolewa kwa mshindi wa kampeni ya benki hiyo inayofahamika ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’inayolenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana kupitia benki hiyo. Wengine ni pamoja na Wengine ni ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bi Neema Tatock (wa pili kushoto) na maofisa wa benki hiyo.
Meneja Masoko na Mawasiliano Msaidizi wa Benki ya Exim Bi Mariamu Mwapinga (Katikati) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’ inayolenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana kupitia benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bi Neema Tatock (Kulia) na Ofisa Bidhaa za Rejareja, Callist Butinga (Kushoto)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...