Mwandishi Wetu,
Dar
es Salaam. Joto la mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East
Africa 2021 limeanza kupanda ambapo washiriki wa mashindano hayo
wataanza kuingia Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii.
Makamu wa
Rais wa mashindano hayo, Jolly Mutesi amesema washiriki hao wapo tayari
kwa maandalizi ya mwisho ambapo fainali ya mashindano hayo
yanayosubiliwa kwa hamu kubwa itafanyika Desemba 17, 2021 katika ukumbi
wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam
Amesema kwamba msanii
Mboso wa Tanzania ni mmoja wa wasanii wakubwa watakaotumbuiza katika
mashindano hayo yanayotarajiwa kuangaliwa na mamilioni ya watu barani
Afrika LIVE kupitia katika Television na Internet Duniani kote.
Nchi zinazoshiriki mashindano ya Miss East Africa ni pamoja na Kenya, Uganda,
Rwanda, South Sudan na Somalia. zingine ni Reunion, Ethiopia, Malawi, Burundi na Mauritius.
Kiingilio cha chini katika mashindano hayo ni Tsh 50,000 kwa tiketi za kawaida na Sh100,000 kwa VIP na Tsh200,000 kwa VVIP
Mashindano
ya Miss east Africa yanaandaliwa na kampuni ya Rena Events kwa
kushirikiana na Wasafi Media.“Tanzania itawakilishwa na Mrembo Queen
Mugesi ambae aliwashinda warembo zaidi ya 2,600 wa Tanzania walioomba
kuiwakilisha nchi kwa njia ya mtandao ambapo Queen Mugesi alichaguliwa
katika mchakato ulioendeshwa na wataalamu wa mambo ya urembo kwa zaidi
ya mwezi mmoja,” alisema.
Alisema, mashindano ya Miss East Africa
ambayo yaliasisiwa na Mtanzania Rena Callist mwaka 1996, yanasubiriwa
kwa hamu kubwa na wapenzi wa mambo ya urembo na yanatarajiwa kuangaliwa
na zaidi ya watu milioni 200.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...