Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


KLABU ya Biashara United Mara rasmi imetupwa nje ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu wa 2021-22 baada ya kushindwa kusafiri kwenye mchezo wao wa mkondo wa pili dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya mchezo uliokuwa uchezwe Oktoba 23, 2021 kwenye dimba la Martyrs Benina mjini Benghazi.

Taarifa ya iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutoka Shirikisho la Soka barani (CAF) imeeleza kuwa Shirikisho hilo lilipokea malalamiko ya timu hiyo kutoka Tanzania, kushindwa kufika nchini Libya. CAF imeeleza kuwa malalamiko hayo yalipelekwa kwenye Kamati ya Mashindano ya ngazi ya Klabu kwa ajili ya utatuzi, baadae ilionekana malalamiko hayo hayana mashiko kuzuia timu hiyo kusafiri hadi Libya.

Kufuatia hatua hiyo, CAF imeeleza kuwa Biashara United imeshindwa kufuzu hatua ya mtoano (PlayOff) ya Michuano hiyo kulingana na ibara ya 16, Sura ya XI ya Kanuni zinazoendesha Michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Hata hivyo, taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mashindano ya CAF, Samson Adamu haikueleza kufungiwa Biashara United kushiriki Mashindano hayo wala kutozwa faini yoyote kutokana na kushindwa kufika kwenye mchezo wao dhidi ya Al Ahly Tripoli nchini Libya.

Al Ahly Tripoli rasmi wanafuzu hatua inayofuata ya mtoano kuwania kuingia makundi ya Michuano hiyo, watacheza na Stade Maliƫn ya Mali.

Biashara United ilishindwa kufika nchini Libya kwa sababu zilizoelezwa kukosa kwa wakati vibali vya Kimataifa vya Anga katika nchi za Sudan, Sudan Kusini na Libya. Mchezo wa mkondo wa kwanza Biashara United ilishinda bao 2-0 kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Oktoba 15, 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...