Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa akifungua mkutano wa makandarasi wazalendo mkoani Iringa jana kuhusu ujuzi wa biashara. Kushoto ni Meneja wa CRB, Kanda ya Kusini Mhandisi Ally Mwita na Mratibu wa mafunzo CRB Neema Fuime. Kulia ni Naibu Msajili CRB, David Jere
Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa akiwasili kwaajili ya kufungua mkutano wa makandarasi wazalendo mkoani Iringa jana kuhusu ujuzi wa biashara. Kushoto ni Meneja wa CRB, Kanda ya Kusini Mhandisi Ally Mwita na Mratibu wa mafunzo CRB Neema Fuime. Kulia ni Naibu Msajili CRB, David Jere
Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa akiwa kwenye picha ya pamoja na makandarasi wazalendo mara baada ya kufungua mkutano wa siku tatu kwa makandarasi wazalendo mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa akizungumza na Mratibu wa Mafunzo wa bodi ya makandarasi (CRB), Neema Fuime kushoto na kulia Msajili Msaidizi wa CRB, David Jere baada ya kufungua mafunzo kwa makanadarasi wazalendo mkoani Iringa.
Na Mwandishi Wetu, Iringa

MAKANDARASI nchini wametakiwa kuisoma mikataba kwa umakini mkubwa kabla ya kuisaini ili kuepuka kuingia kwenye mikataba ambayo wanaweza kushindwa kuitekeleza na kukimbia miradi wakati wa kuitekeleza.

Hayo yamesemwa leo Novemba 3, 2021 mjini Iringa na Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Consolata Ngimbwa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa makandarasi wazalendo wa nyanda za juu kusini mkoani Iringa kuhusu usimamizi wa biashara.

Mhandisi Ngimbwa amesema ni vyema mkandarasi akajiridhisha na mkataba anaoingia kwa kuusoma vizuri na kama haelewi kuomba ufafanuzi ili asijiingize kwenye mkataba ambao hataweza kuutekeleza.

Amesema baadhi ya makandarasi wamekuwa wakiwapa watu hasa wahandisi kuwajazia zabuni hali ambayo imesababisha wakose zabuni hizo kutokana na kujazwa bila kufuata taratibu.

“Msiwape watu wengine wawajazie na mkipata zabuni msome mikataba kwa umakini msikimbilie kusaini tu mwishowe mnalalamika kumbe yale mliyolalamikia yalikuwepo wakati unasaini,” alisema

“Unakuta kwenye zabuni umeambiwa ueleze uzoefu wa miaka mitano wewe unajaza uzoefu wa miaka mitatu halafu unasubiri upate zabuni na ukikosa unalalamika wakati hukukidhi vigezo,” amesema Mhandisi Ngimbwa.

Pia amewataka makandarasi kuungana ili waweze kuwa na nguvu ya kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi kwani hata makampuni makubwa ya wachina yamekuwa yakiungana kwaajili ya kutekeleza miradi mikubwa.

Amesema makandarasi wengi wamekuwa wakiogopa kuingia kwenye kufanya kazi kwa ubia kwa kuhofia kupata hasara lakini alisisitiza kuwa ubia haukwepeki kwani ndiyo jawabu la mafanikio ya makandarasi wazalendo.

“Kazi za ubia zinachanagamoto zake lakini msiogope kufanyakazi kwa umoja kwasababu ukiwa kwenye ubia kuna mambo mengi unajifunza na unapata uzoefu wa kutosha kufanya miradi mikubwa,” alisema

Amewataka pia kuachana na utaratibu wa kuwa na vyama vingi vya makandarasi na kuanzisha chama kimoja chenye nguvu ambacho kitakuwa sauti yao wanapokuwa na matatizo na changamoto mbalimbali kwa serikali au kwa wateja wao.

Amewataka makandarasi pia kujifunza kujaza zabuni kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa serikali wa TANePs ambao ndio unatumika kwa sasa kujaza zabuni za serikali.

Amesema kwa kuwa mtoaji wa zabuni nyingi ni serikali hakuna namna ambayo makandarasi haao wanaweza kukwepa kuujua mfumo huo kwani zabuni zote za serikali zinaombwa kupitia mfumo huo wa kielektroniki.

Meneja wa CRB nyanda za juu kusini, Mhandisi Ally Mwita alisema wateja wanapaswa kuwalipa makandarasi kwa wakati ili waweze kutekeleza miradi wanayopewa kwa wakati uliopangwa na kwa ufanisi.

“Umempa mkandarasi zabuni ametumia fedha zake na amekamilisha unapaswa kumlipa kwa wakati ili nayeye alipe wanaomdai na kushindwa kufanya hivyo ni kumdhoofisha mkandarasi.” Amesema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...