WAZIRI MKU
Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania pamoja na wadau wa soka nchini kuungana kwa pamoja na kuhakikisha timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa Miguu (Taifa Stars) inafanya vizuri kwenye michezo yote iliyobaki ili kufuzu kushiriki kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022.

 

Ametoa wito huo leo (Alhamis, Novemba 4, 2021) wakati akiongoza Kikao cha pamoja cha wadau wa soka Nchini katika ukumbi wa uwanja wa Taifa wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Ambapo katika kikao hicho wadau wa Taifa Star wamechangia Shilingi Bilioni 1.6 ambazo zitatumika kuihudumia timu katika maandalizi ya mechi zilizobaki za kufuzu kombe la Dunia.

 

Akizungumza kwenye kikao hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema ni lengo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anakuza sekta ya michezo nchini na anataka kuona mafanikio katika timu za Taifa hivyo mikakati ya kuifanya timu ya Taifa ifanikiwe ni sehemu ya kutimiza malengo ya Mheshimiwa Rais.

 

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda, Taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau wengine kuendelea kujitokeza kuichangia timu ya Taifa ili iweze kuweka Historia ya kushiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

 

Wadau Walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na GSM, TAIFA GAS, AZAM, CRDB, NBC, LAKE OIL, STAR OIL, K4 SECURITY, KAMBIASO pamoja na wadau wengine.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...