Na Khadija Kalili
Mkurugenzi wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi (City College of Health and Allied Sciences) Shaban Mwanga ametoa wito kwa wanafunzi wa Chuo hicho na jamii kuchangia damu Ili kusaidia Kituo Cha Afya Cha mama na mtoto iliyopo Chanika Ilala Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo alisema hayo leo alipokuwa akiongoza zoezi la kuchangia damu lilofanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho ikiwa ni katika kilele cha kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa tawi la hilo la Chanika.
" Nawahamasisha wakaazi wote wa Chanika , wanafunzi wa Chuo changu wajitokeze kwa wingi katika kuchangia damu kwa sababu itasaidia kuokoa maisha ya wahitaji wengi hasa mama na mtoto kama tujuavyo kwenye wodi za kina mama na watoto ambapo damu nyingi huhitajika" alisema Mwanga.
Akizungumza kwa niaba Mkuu wa Kitengo Cha Damu Salama Mkoa wa Ilala Bernadetha Mshima alisema kuwa uchangiaji wa damu una faida kwa jamii pia ni ibada kiimani kwani kila mtu anayetoa damu huwa hafahamu itakwenda kumsaidia nani.
Hafla hiyo ilikua ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...