Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wakili Msandi amebainisha hayo leo katika siku ya pili ya tamasha la Njombe ya Mama Samia linaloendelea katika kituo cha zamani cha mabasi cha Njombe mjini na kusema kuwa wakazi wengi wanakata tamaa kwa kuona mizunguko mirefu wakati wa kutafuta haki mahakamani badala ya kuwatafuta wanasheria ili waweze kuwasaidia kutatua changamoto hizo.
“Mpaka sasa tumeshawahudumia wananchi wapatao 33 wakiwa na shida mbali mbali ya ardhi,ndoa,mirathi na kazi na kwa namna ya kipekee tumegundua mkoa wa Njombe ni kuto kuwa na uelewa kwa wananchi kwasababu wengi wamekuja wakiwa na mashauri yanayotakiwa kwenda mahakamani lakini kwa bahati mbaya muda wao wa kwenda mahakamani umeshapita”alisema Msandi
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa baada ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanyika katika mabanda mbalimbali amesema tamasha hilo limesaidia sana kuwasogezea wananchi huduma karibu na kwa urahisi kwani zimekuwa zikitolewa kila siku katika ofisi za serikali.
“Wananchi mwitikio wao ni mzuri na tunaendelea kuwapa huduma na kwa kweli watu wanatoka mpaka wilaya za karibu kwa kweli inatia faraja”alisema Kissa Kasongwa
Tamasha la Njombe ya Mama Samia lililoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Njombe linafikia tamati kesho Novemba 17 mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa akizungumza na waandishi wa habari leo katika siku ya pili ya tamasha mara baada ya kutembelea mabanda yaliyopo kwenye tamasha hilo na kuona shughuli zinavyoendelea.
Baandi ya wananchi waliofika katika banda la wanasheria wakiendelea kupata msaada wa kisheri.
.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...