Benki ya Equity (T)
imetia saini Mkataba wa Makubaliano na Shirika la Posta nchini kutumia
vituo vya Shirika hilo kutolea huduma za kibenki ili kusogeza
huduma karibu na watanzania wengi zaidi.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Robert Kiboti
amesema “Hatua hii itatuongezea wigo wa
mtandao wa utoaji huduma zetu ambazo ni nafuu zaidi nchini na hivyo
kuendana na lengo letu la kukomboa Watanzania kiuchumi kwa
kuongeza ushiriki wao katika mfumo rasmi wa fedha (financial inclusion).
“Kwa sasa Equity Bank ina mawakala wapatao 3,900 na hivyo kuungana
na Shirika la Posta kuwa kama Supa Wakala wetu , kupitia mtandao wa
ofisi zake  kutatuwezesha kuongeza idadi ya watu
watakaofikiwa na huduma zetu kwa ukaribu na urahisi zaidi. Kwa
kuanzia tutaanza na vituo 35 kwa maeneo ambayo hatukuwepo hapo awali" alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta
Tanzania, Macrice Mbodo amesema  “Tunajivunia kuweza kuungana na Benki ya Equity
katika kufanikisha mpango huu utakaosaidia kufikisha huduma za
kibenki kwa Watanzania wengi zaidi. Juu ya hilo kupitia mpango huu
Shirika la Posta pia litapata chanzo kipya cha mapato kupitia kamisheni
na hivyo kuimarisha mapato ya shirika”. Amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Robert Kiboti akitia saini Mkataba wa Makubaliano na Shirika la Posta nchini. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Robert Kiboti na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta
Tanzania, Macrice Mbodo Wakikabidhiana Mkataba huo.


 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...