MAPEMA leo Chuo cha Maji na Mamlaka ya Maji Zanzibar wameingia katika historia kubwa ya kukubaliana na kusaini Mkataba wa Makubaliano ( Memorandum of Understanding) katika kuanzisha na kuendeleza mashirikiano katika masuala ya Mafunzo, Utafiti, Ushauri wa Kitaalam na Ubunifu.
Lengo ni kuhakikisha Mamlaka ya Maji Zanzibar inanufaika na uwepo wa Chuo cha Maji lakini pia Chuo kinafaidika na fursa zilizopo katika Mamlaka hiyo na kuhakikisha ile Zanzibar ya Blue inafikiwa kwa mafanikio ya haraka yatakayosaidia Taasisi hizi kufanya mabadiliko chanja kwa haraka zaidi.
Mkuu wa Chuo Dkt. Adam O. Karia na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Dkt. Salha Kassim wamesaini mkataba huo tayari kuanza kushirikiana mara moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...