Na Amiri Kilagalila,Njombe
MKUU wa wilaya ya Njombe ya Njombe Kissa Kasongwa ameandaa tamasha ambalo litakutanisha mawakili 20 kutoka mkoa wa Njombe na Iringa wanatarajiwa kutoa msaada wa kisheria siku tatu mfululizo kwa wananchi wa wilaya ya Njombe wanaokabiliwa na kero ya migogoro ya ardhi,ndoa pamoja na mirathi.
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa mawakili hao amesema mawakili hao wanakuja kufuatia ofisi yake kupokea malalamiko ya migogoro hiyo hasa ya ardhi mara kwa mara hivyo ikamlazimu kuandaa tamasha ambalo litakutanisha mawakili,wananchi pamoja na wajasiliamali katika uwanja wa sabasaba.
‘’Tumeandaa tamasha kuanzia tarehe novemba 15 hadi 17 ambalo tumeita wanasheria wa kujitolea mawakili ambao wanatokea mkoa wa Iringa na Njombe kama 20 ambao watatoa msaada wa bure kabisa wa kisheria kwa wananchi ’’amesema Kasongwa.
Aliongeza kuwa’’Tumeamua kufanya hivyo kwa sababu tumeona wananchi wa wilaya ya Njombe wanasumbuka sana na migogoro ya ardhi,ndoa na miradhi na inapelekea matukio mengine kutokea kutokana na kushindwa kumalia matukio yao au zile kesi’’amesema mkuu wa wilaya.
Mkuu wa wilaya amesema kuwa wananchi wa Njombe wakitumia vizuri fursa hiyo itasadia kuepuka migogoro mingi ambayo ipo kisheria ambayo haitatuliwi kwenye upande wa siasa.
‘’Tamasha hili ambalo tumeliandaa litasindikizwa na vitu vingi kama huduma kutoka taasisi zote kutoka tasisi zote za serikali ziliopo wilaya ya Njombe,kutakua na mifuko ya kijamii,tasisi binafsi pia kutakua na huduma za upimaji afya bure kwa magonjwa yote kwa hiyo wananchi wakaribie ili waweze kuja kuona kitu gani ambacho tumewaandalia’’amesema Kasongwa.
Pia alisema ‘’Mh Raisi wetu mama Samia Suluhu Hassan katika msisitizo wake anatuelekeza sisi wasaidizi wake kutatua kero za wananchi na asingependa anapopita kwenye ziara zake na wananchi akute wanakero au kuna vitu ambavyo havijatatuliwa,ndo maana tunafanya kila linalowezekana pamoja na kuwafikia kwenye maeneo yao tunafanya ubunifu ili wananchi waweze kutatuliwa wengi kwa wakati mchache ili iweze kuleta tija kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu’’amesema.
Pia mkuu wa wilaya ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo ambapo licha ya mawakili hao pia kutakua na fursa ya wajasiriamali kuonyesha bidhaa zao bure hivyo uandikishaji utafika novemba 13 uwanja wa sabasaba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...