Rais wa Internet society tanzania (ISOC), Nazar Kilama akizungumza kuhusiana Majadiliano ya Internet kwa Vijana (YIGF) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa Mafunzo kwa Vijana, Essa Mohamedali akitoa mafunzo kwa vijana wq chuo kikuu cha Dar es Salaam na wengine walioko mtandaoni juu ya Majadiliano ya Internet Kwa Vijana (YIGF).
Katibu na Mwezeshaji wa Majadiliano ya Internet kwa Vijana (YIGF), Evelyn Rujuguru akizungumza na vijana wenzie kuhusiana na umuhimu wa masuala ya Internet ya kutoa majawabu kwa jamii
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Moses Ismail akizungumza kuhusiana na teknolojia ya mawasiliano namna ya vijana wanavyohitaji mafunzo kwenye majadiliano ya internet kwa vijana( YIGF).



Baadhi ya vijana wakiwa katika mafunzo ya majadiliano ya Internet kwa Vijana (YIGF).

*Yaanzisha majadiliano ya Intenet kwa vijana vyuo vikuu.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
INTERNET Society Tanzania (ISOC) imesema kuwa vijana ni taifa la leo hivyo wanahitaji kuwa na uelewa wa Internet na kuweza kuwa wasimamizi wazuri pamoja kutoa suluhu kwa jamii.

Akizungumza katika majadiliano ya kwanza Vijana katika masuala Internet (YIGF) Rais Internet Society Tanzania (ISOC) Nazar Kilama amesema kuwa vijana wa vyuo wana uwanja mpana katika kufikisha elimu juu ya matumizi ya mtandao na kuja kutoa suluhu katika jamii inayozunguka hususani katika matumizi salama mtandao.

Kilama amesema kuwa katika majadiliano hayo wameanza na wanafunzi wa vyuo vikuu katika ambao wanasoma masuala ya komputa ili kuweza kutambua umuhimu kuendeleza majadiliano mengi kwa vijana katika matumizi ya internet na mtandao.

Amesema nchi imejenga miundombinu ya mawasiliano ili kuweza kutumiwa na watanzania ambapo miundombinu hiyo inahitaji watu wa kuendeleza na kulinda katika matumizi.

Aidha amesema internet inaunganisha watu wengi wa ndani na nje hivyo elimu na majadiliano yanatakiwa kuwa endelevu zaidi na hakuna kujitenga kwani ukiacha wengine wanaendelea kujadili .

Kwa upande wa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Moses Ismail amesema kuwa internet na mitandao inaunganisha watu wengi hivyo kunatakiwa vijana kuwa sehemu ya kutoa elimu juu ya matumizi hayo.

Amesema kuwa teknolojia inabadilika kila siku ambapo kunahitajika kuendelea kuwepo kwa watafiti ambao wataendelea kufanya eneo hilo.

Katibu na Uwezeshaji (YIGF), Evelyn Rujuguru amesema vijana ni sehemu kubwa ya watumiaji wa internet hivyo wanatakiwa kujua vitu gani vya kufanya au kuacha.

Amesema kuwa wakati mwingine internet inatoa fursa ya ajira kwa kuomba kazi kupitia mtandao au kufanya biashara ndani ya mtandao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...