Kwa mujibu wa wataalamu wa Afya, chanjo za COVID-19 zinafanya kazi kama chanjo nyingine. Chanjo husaidia mwili wa mtu kutambua na kupambana dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa. Chanjo ya COVID-19 husaidia mwili kutambua na kupambana na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.
Je! Chanjo za COVID-19 zinatulinda jinsi gani?
Chanjo za COVID-19 hufundisha mwili wako kutambua na kupambana na virusi vya COVID-19. Hazina COVID-19. Huwezi kupata ugonjwa wa COVID-19 kutoka kupata chanjo. Chanjo ni njia salama ya kujenga kinga dhidi ya virusi katika mwili, bila kusababisha ugonjwa. Chanjo za COVID-19 ambazo zilipitishwa kwa matumizi zimeonyeshwa kuwa nzuri sana katika kulinda dhidi ya ugonjwa mkali na kifo.
Unaweza kuzungumza na daktari wako juu ya chanjo za COVID-19 na kwa nini chanjo ni sehemu muhimu ya kuitunza jamii kuwa salama na yenye afya.
Je! Nitarajie madhara gani kutoka chanjo za COVID-19?
Chanjo zote zinaweza kuwa na madhara kadhaa. Madhara haya kwa kawaida ni kidogo na hudumu kwa siku chache tu. Madhara ni pamoja na: • mkono wenye maumivu baada ya sindano • homa • kuumwa kwenye misuli • kuumwa kichwani. Hizi ni ishara kuwa chanjo inafaa. Kama una maswali yoyote au wasiwasi baada ya chanjo, wasiliana na kliniki yako ya chanjo au daktari yako.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...