Chanjo za COVID-19 ni nzuri sana, bure, salama na zenye ufanisi.
Baada ya kupewa chanjo kamili, unaweza kuendelea na shughuli ambazo ulifanya kabla ya janga hilo.
Kila mtu mwenye umri wa miaka kumi na mbili na zaidi sasa anastahiki kupata chanjo ya COVID-19.
Hatari kutoka kwa Ugonjwa wa COVID-19 • COVID-19 imeua zaidi na karibu wote hao ambao walikuwa hawajachanjwa • Hata wale walio katika hatari ndogo ya kifo kutokana na COVID-19 wanaweza kupata matokeo ya muda mrefu.
Faida za Chanjo za COVID-19
Ukiwa umepewa chanjo kamili ya COVID-19, kuna hatari ndogo ya kuambukizwa na COVID-19.
Chanjo zina ufanisi wa hadi asilimia 95 katika kuzuia maambukizi ya dalili ya COVID-19. Hata ukipata COVID19, kuna hatari ndogo sana ya ugonjwa mbaya au kufa.
Unaweza kusaidia kuweka watu karibu na wewe salama.
Chanjo pia husaidia kupunguza kuenea kwa COVID-19 kwa wengine walio katika hatari ya kuambukizwa sana.
Unaweza kufanya mambo Zaidi. Baada ya kupata chanjo kamili, ni salama kufanya vitu kama kumtembelea rafiki aliyepewa chanjo.
Unaweza kutembelea nchi zingine bila kupimwa COVID-19.
Usalama wa Chanjo za COVID-19
Chanjo zimechunguzwa kwa karibu na zinaonekana kuwa salama sana.
Chanjo huchunguzwa vizuri kabla na baada ya kutolewa kwa umma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...