KAMPUNI bora ya huduma za mziki mtandaoni ya Mdundo Records imeweka rekodi ya kipekee Barani Afrika baada ya kufikisha idadi ya watumiaji milioni 16.4 kipindi cha robo tatu cha mwaka wa 2021, kilichoishia Septemba mwaka huu.

Matokeo hayo ni ongezeko la asilimia 10 ikilinganishwa ni robo iliyotangulia, ambapo ongezeko hilo limechangiwa na idadi kubwa ya watumiaji wapya kutoka nchi za Tanzania, Kenya na Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, Tanzania iliongoza kwa kuwa na watumiaji wapya katika robo tatu ya mwaka ambapo jumla ya watumiaji wapya 4.1 waliripotiwa, huku Nigeria na Kenya zikirekodi watumiaji wapya milioni 3.1 na milioni 2.6 mtawalia.

Nchini Tanzania, kampuni ya Mdundo records ilikua kwa asilimia 36 kutokana na watumiaji wapya milioni 4.1 hivyo kuchangia asilimia 24 ya jukwaa la watumiaji wa kampuni hiyo katika kipindi hicho cha robo tatu ya mwaka wa 2021.

Akizungumzia mafanikio hayo, Mkuu wa Mdundo Brand Partnerships Africa, Rachel Karanu alisema,

“Mafanikio haya ambayo yamekuwa kwa kasi kubwa ni ushahidi tosha kuwa taasisi yetu ni kichocheo dhabiti katika kukuza biashara kwa kuvutia wateja zaidi kupitia kitengo chetu cha matangazo cha Mdundo For Brands.

Tunafanya kazi kwa karibu sana na chapa zinazoongoza kibiashara Barani Afrika hivyo mafanikio haya ni habari njema kutokana na ukweli kwamba chapa ya Mdundo na wateja wetu inawafikia wateja wengi sana Barani kote”.

“Tunatarajia kukuza wigo wa jukwaa letu kwa kuwafikia wateja wengi zaidi katika robo ya mwisho ya mwaka 2021, hivyo kuongeza thamani za bidhaa za wateja wetu”, alisema.

Kwa mujibu wa uongozi wa taasisi hiyo, kampuni hiyo inafanya kazi na baadhi yenye chapa bora za kibiashara katika nchi za Kenya, Nigeria na Tanzania.

Katika kipindi cha robo tatu cha mwaka, kampuni hiyo imeweza kushughulikia ukuaji wa chapa wa makampuni bora Barani Afrika ambayo ni pamoja na Sportpesa, Safaricom, Chrome Gin, Standard Chartered Bank, Captain Morgan, Coca Cola, BetKing na Guinness Smooth kwa kutaja machache.

Miradi ya chapa imejikita kwenye vifaa vipya vya kuboresha chapa iliyozinduliwa hivi karibuni ya Mdundo Brand Lift Tool na ambayo inapatikana bila malipo pia inatoa bila malipo taarifa muhimu kuhusiana wateja na chapa zao.

Kupitia Mdundo Brand Lift Tool, Mdundo imefanikiwa kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa wakati huku ikitoa taarifa ya mafanikio ya kampeni zake kwa wateja wake zinazohusiana mafanikio ya chapa zao yanayotokana na uhamasishaji kupitia matangazo mbalimbali.

Haya yote yanatafsiri isiyopingika ya kuwa Mdundo inakuwa na data katika kukuza chapa zao, amapo moja wapo ya chapa inayoongoza Barani Afrika ya Vodacom ilipata mafanikio makubwa baada ya mauzo yake kukua kwa asilimia 76 baada ya kufanya matangazo yake kupitia kampuni ya Mdundo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...