JESHI la Polisi nchini limeelezea uwepo wa makosa ya udhalilishaji kwenye jamii na likitaja kupungua kwa vitendo hivyo katika baadhi ya maeneo huku maeneo mengine udhalilishaji ukitajwa kuongezeka.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Dkt. Mussa A. Musssa wakati akifungua mkutano wa tatu wa Makamishna na Makamanda wa Polisi wa Mikoa Tanzania katika kuimarisha upatikanaji wa haki jinai kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.
Aidha,Dkt. Mussa, amesisitiza kuwa, Jeshi la Polisi litaendelea kujikita katika kuandaa mipango mbalimbali ili kutatua changamoto walizonazo wananchi ikiwemo makosa yanayotokana na ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto bwana Koshuma Mtengeti amesema kuwa, kwa muda wa miaka kumi sasa wamekuwa wakishirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha wanashughulikia kesi za ukatili wa kingono na makosa mengine dhidi ya watoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...