Na Mwandishi Wetu,Milena
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewataka Umoja wa vijana wa chama hicho kuacha tabia ya kuwa wapambe wa wagombea na badala yake wajikite katika kufanya kazi ya kujenga nchi Kwa kujitolea.
Akizungumza leo Novemba 15,2021,Chongolo Amesema kwamba kwa sasa vijana wengi wa umoja huo wamekuwa wapambe namba moja wa wagombea na wahangaikaji wa mambo binafsi ya viongozi na kuacha majukumu yao halisi
Amesema malengo ya kuanzisha umoja wa vijana haikuwa na maana ya kuwatumia vijana hao kwenye mambo ya kutafuta kura za wagombea bali ni kujenga nchi kwa kujitolea na baadae kupata fursa ya kwenda kulitumikia taifa kwa faida yao na nchi.
Ameongeza miaka ya nyuma kazi ya umoja wa vijana ilikuwa ni kujiitolea kujenga miundombinu na kufanya mambo mengine ya maendeleo na baadae kupata fursa ya kwenda jeshini kulitumikia taifa kwa faida yao na nchi kwa ujumla.
“Miaka ya 2000 nyuma, asilimia tisini ya vijana ambao walikuwa wanachukuliwa kwenda jeshini walikuwa wanatokana na umoja wa vijana na ni kwa sababu walikuwa wanajitolea kulitumika taifa kwa kupitia umoja huo,” amesema.
Katika hatua nyingine, Chongolo amewapongeza umoja wa vijana Wilaya ya Muleba Kwa kujitolea kujenga vyumba vya madarsa katika shule ya Bukama Wilayani Muleba.
Chongolo amemtaka mwenyekiti wa halmashauri pamoja na viongozi wa Muleba kuendelea kuwatumia vijana hao katika kujenga miundombinu mingine.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Ndugu Elias Kayandabila mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya Sekondari Bukama Kata ya Kagoma ambapo vijana zaidi ya 90 wa wilaya ya Muleba wameweka kambi na kujitolea katika kazi za kimaendeleo. (Picha na CCM Makao Makuu)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...