ZIKIWA zimepita siku chache, Rais Samia Suluhu kutoa agizo kwa Wakuu wa mikoa kufatilia vyanzo vya Maji vilivyochepushwa, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es Salaam imefanya ziara katika Mtambo wa Kuzalisha Maji wa Ruvu Juu na Chini ili kujionea Changamoto ya uzalishaji Maji baada ya kufanyika operesheni za kufungua njia za mito.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Amos Makalla amesema baada ya kufanyika kwa oparesheni hiyo katika mto Ruvu changamoto iliyobaki ni kukosekana kwa mvua katika msimu huu hali ambayo imechangiwa na mabadiliko ya tabianchi hivyo akatumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa Dar es Salaam na Pwani kumuomba Mungu mvua zinyeshe ili kuondoa ukame uliopo lakini akasisitiza kutunza vyanzo vya maji na kutumia vizuri maji yaliyopo.

Aidha Makalla ameweka bayana kiasi cha Lita zinazozalishwa kwa sasa katika Mtambo wa Ruvu Chini kuwa ni milioni 200 kwa siku ikilinganishwa na awali Lita milioni 270 kwa siku hivyo kuna upungufu wa Lita milioni 70.

Pia amewataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Meya wa Manispaa pamoja na jiji la Dar es Salaam kuwa mabalozi wazuri hasa kwenye kipindi hiki cha mgao hivyo wanapaswa kufikisha ujumbe kwa wananchi wao ili kuweza kupunguza maneno yasiyokuwa ya kweli kwenye jamii.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema anaishukuru Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kutembelea mitambo ya kuzalishia maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kujione hali iliyopo kwasasa kwenye mto Ruvu.

Amesema ugeni huu ni kuonesha kuwa Serikali iko karibu na DAWASA kwenye kipindi hiki cha upungufu wa maji katika mto Ruvu hivyo kuona kwao ndo wanaweza kusema kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, wakuu wa Wilaya Pamoja na viongozi wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Afisa mtemdaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaonesha kina cha maji kwenye mto Ruvu wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ya kutembelea na kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu leo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla , wakuu wa Wilaya Pamoja na viongozi wa Ulinzi na Usalama kuhusu kazi zinazofanywa kwenye Mtambo wa kusukumia wa maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ya kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla , wakuu wa Wilaya Pamoja na viongozi wa Ulinzi na Usalama kuhusu namna uzalishaji wa maji wa Ruvu Juu chini ya usimamizi wa DAWASA wakati wa Ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ya kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla wakiendelea kukagua na kujionea uzalishaji maji katika Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kutembelea  na kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu leo Mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza na wandishi wa habari kuhusu namna walivyojipanga kusimamia na kulinda vyanzo vya maji ikiwemo Mto Ruvu unaotoa huduma ya Majisafi na salama kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Pwani wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ya kutembelea na kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu leo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna DAWASA inavyopambana kuweza kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji pamoja na kumaliza mgao wa maji wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Pwani wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ya kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...