Na Mwandishi Wetu, Michuzi Blog 

KIWANDA cha Keko Pharmaceutical (KPI), kimeomba serikali ikipatie mtaji endelevu ili kuwa na uzalishaji endelevu unaokidhi mahitaji ya nchi.

Mtaji huo utasaidia  kuongeza uagizaji wa malighafi, kuboresha miundombinu ya kiwanda hicho ili kukidhi viwango vya kimataifa (cGMP)

Pia, kiwanda hicho pamoja na kuzalisha kwa sasa dawa zinazotosheleza mahitaji na ziada nchini, kina mpango wa kuongeza uzalishaji wa aina  nyingine za dawa  kutoka dawa 10 zinazozalishwa hivi sasa kufikia aina 15 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2022.

Dawa zinazozalishwa Kiwanda cha Keko ni miongoni mwa orodha ys dawa muhimu zinazopatikana katika kitabu cha mwongozo wa matibabu nchini na mahitaji yake ni makubwa kwani zinatibu magonjwa 10 ya kipaumbele nchini.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kiwanda hicho Betia Kaema mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Alisema kutokana na ukosefu wa mtaji endelevu kwa sasa kiwanda hicho kinashindwa kuagiza malighafi na vifungashio vya kutosheleza uzalishaji wa miezi 3 na zaidi

Pia kushindwa  kuboresha miundombinu ya kiwanda kufikia kiwango cha kimataifa na kuongeza mashine zaidi ili kupanua uwezo wa uzalishaji.

Alifafanua pia kuwa  changamoto nyingine ni ongezeko la kodi kwa baadhi ya vifungashio na vipuri vya mashine za uzalishaji zinazoagizwa nje ya nchi. Vifungashio hivi havina msamaha wa kodi na hivyo husababisha gharama za uzalishaji kuwa juu

Hata hivyo, alielezea mafanikio ya kiwanda hicho tangu kuanzishwa kwake miaka 53 hadi sasa, kuwa kilikuwa kinazalisha dawa moja lakini katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Oktoba mwaka jana kinazalisha dawa aina 10.

Malengo ni kupanua kiwanda hiki kuwa cha kisasa zaidi na kuongeza aina za dawa zinazoweza kuzalishwa.  Na kukiboresha kufikia viwango vya uzalishaji wa kimataifa  ili kukiongezea thamani na kuleta chachu kibiashara sokoni,” alisema Kaema.

Alisema dawa 10 zinazotengenezwa ni zile zilizoidhinishwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ambapo dawa mbili ni kwa ajili ya kutibu magonjwa ya maumivu, aina saba ni za kutibu magonjwa yatokanayo na maambukizi ya vimelea vya bakteria (antibiotics) na aina moja ni kwa ajili ya magonjwa yanayosababishwa na fangasi.

Alitaja dawa 10 zinazotengenezwa kwa sasa kuwa ni Paracetamol, Metronidazole, Erythromycin, Ampiclox, Pen V,  Amoxicillin, Co-trimoxazole, Griseofulvin, Ciprofloxacin na Paracetamol + Diclofenac

Alisema kwa sasa kiwanda hicho kina uwezo wa kukidhi  asilimia 100 za mahitaji ya nchi kwa aina ya dawa zinazozalishwa.

“Matarajio yetu ya baadaye ni kuongeza mashine zaidi ili kupunguza muda wa uzalishaji ili kuleta ufanisi zaidi lakini pia kufanya ukarabati wa kila mara kwa mashine zinazosuasua ili uzalishaji usisimame,” alieleza Kaema.

Mkurugenzi alimalizia kwa kutoa wito kwa Watanzania kupenda kutumia dawa zinazozalishwa ndani ya nchi kupitia viwanda vinavyosimamiwa na Wazawa Watanzania. Tofauti na sasa ambapo walio wengi wanaamini dawa zinazozalishwa nje ya nchi ndizo zenye ubora na viwango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...