Ni ya mtoto anayekunywa maji machafu katika dimbwi.

       Wapotoshaji wameitumia kwa namna mbalimbali ikiwemo kumuhusisha Hayari Rais Magufuli.

Na.Vero Ignatus,Arusha

Mitandao ya kijamii imeendelea kuwa nyenzo kuu ya mawasiliano ya watu lakini wapo ambao wanaitumia vibaya kupotosha umma kwa ajili kujipatia fedha au kusababisha madhara mbalimbali ya kiafya na kijamii.

Hivi karibu katika mtandao wa Facebook imekuwa ikisambazwa picha ya mtu ambaye yuko kwenye dimbwi la maji machafu (rangi ya kahawia) akiwa na bakuli lake huku akiyanywa.

Picha hiyo inatumika katika matukio mbalimbali ya upotoshaji ikiwemo kumuhusisha aliyekuwa Rais Tanzania, Hayati John magufuli.

Katika upotoshaji uliofanywa Novemba 6, 2021, picha hiyo iliwekewa ujumbe kwa lugha ya Kiingereza unaosema “Ooh Jesus protect this family,I know your so good and Faithful,we are nothing without you Jesus and thanks ooh Lord, type Amen to wish bless of God to all people living in the village without pure water’’

Katika tafsiri isiyo rasmi inasema “Ooh Yesu naomba uilinde hii familia najua wewe ni mwema na mwaminifu,sisi si kitu bila wewe Yesu asante,Andika Amen kwa kuwatakia baraka za Mungu watu wote wanaoishi vijijini bila kuwa na maji safi na salama”

Habari picha hiyo pia imetumika kupotosha kuhusu Hayati Dk Magufuli ambapo mpotoshaji mwingine aliitumia katika mtandao wa Twitter mwaka jana akieleza mambo yasiyo sahihi kuhusu rais huyo aliyeaga duni Machi 17, 2021.


                                                

Aidha, bila kuchoka watu wasio na nia nzuri wameitumia picha katika mtandao wa Twitter Novemba 8 mwaka wakieleza kuwa  ya “kila unapotaka kuiba pesa za nchi, basi uwafikirie na watoto hawa ambao hawana maji safi  ya kunywa tu.”

Kusisitiza kile ambacho wapotoshaji wa mtandao wamekusudia kuhusu picha hiyo wamehusisha na Niger Delta nchini Nigeria ambao wanatumia maji machafu kutoka katika mto wa Egbema Bayelsa.

Upotoshaji huo umefanyika kupitia ukurasa wa Facebook wa IPND ,wenye wafuasi 42,158, mnamo Julai 9, 2019 ambapo imedai kuwa zaidi wakazi milioni 30 wa Niger Delta wanashida ya maji safi na salama hivyo kuwalazimu kunywa  maji machafu.

Habari hizo zina ukweli wowote?

Hakika habari hizo zote zilizohusishwa na hiyo picha hazina ukweli wowote kwa sababu picha hiyo imetumika katika matukio yasiyo sahihi japokuwa ni kweli inaeleza tatizo la maji nchini Ghana.

Kwa kutumia zana za kidijitali ikiwemo Reverse Image Search ya mtandao wa Google na RevEye tumebaini picha hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 21, 2018, ambapo mtumiaji wa mtandao Facebook kutoka Ghana, Genuine Ernest Bishop Ahiabli.

Mtumiaji huyo alikuwa akionyesha hali ya upatikanaji wa maji katika eneo la Akpatoeme, Manispaa ya Ketu Kaskazini ya eneo la Volta nchini humo, ikionyesha watu wanalilia serikali kuomba usaidizi juu ya ukosefu wa maji ya kunywa katika jamii hiyo .

Mwandishi wa habari hii alienda mbali zaidi na kuwasiliana na Ahiabli kupitia ukurasa wake wa Facebook, alithibitisha kuwa alipiga picha hiyo huko Akpatoeme, eneo la mto huo, kwenye picha hiyo ambapo aliweza kutoa picha zaidi, ambazo alichukua siku hiyo hiyo, ili kuthibitisha ni picha yake.

                    Clean water comes to a rural village for the first time.(Maji safi yamekuja kijijini kwa mara ya kwanza)Hii ni moja ya ya picha ya Genuine Ernest Bishop Ahiabli.


                                          

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...